Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu ameendelea na ziara yake Mkoa wa Pwani na leoalikuwa Wilayani Rufiji mkoani humo na kufanya mikutano na kuangalia shughuli za kijamii katika vijiji vya Utete na Ikwiriri.
Hapaanasimulia hali halisi aliyo ikuta Utete
na Ikwiriri - ziara ikiendelea Wilayani Rufiji. Kubwa lililojitokeza ni
idadi ndogo ya wasichana walio ktk shule za sekondari ukilinganisha na
wavulani. Takwimu za Wilaya 2012 zinaonyesha kuwa jumla ya watoto
waliopo ktk shule za msingi ni 50150.
Ke ni 25,292 na Me ni 24858. Cha
kusikitisha uwiano huu hauonekani ktk elimu ya sekondari. Jumla ya
watoto waliopo sekondari ni 9997. Me ni 6455 na ke ni 3542.
Mwamko/hamasa ndogo ya elimu ni mojawapo ya kikwazo kwa wasichana
kuendelea na Elimu ya Sekondari Wilayani Rufiji. Hii inatupa changamoto
kwetu sisi Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Halmashauri
na wadau wa maendeleo ya Wanawake juu ya umuhimu wa kuongeza jitihada
zetu ktk kujenga mwamko na kubadili fikra ktk jamii juu ya UMUHIMU WA
ELIMU KWA WASICHANA. Tanzania itafikia maendeleo ya kweli ya usawa wa
jinsia pale ambapo kutakuwa na uwiano sawa kati ya wanaume na wanawake
kielimu ktk ngazi zote.
Akikagua kazi za ujasiriamali.
Wananchi wakiwa jkatika mkutano wa hadhara.
0 comments:
Post a Comment