Baadhi ya wachezaji wa timu ya Kamba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakishangilia ushindi wao baada ya kuwaburuza timu ya Katiba na Sheria katika raundi mbili mfululizo, katika mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Picha Zote na OMR
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Kamba wakionyesha uwezo wao wa kutunisha misuri kuwaburuza wapinzani wao wa timu ya Katiba na Sheria, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Wachezaji wa timu ya Katiba na Sheria, Kamba wakijaribu kugangamala kuwazuia wapinzani wao wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (kulia), Kamba wakionyeshana umwamba wapinzani wao wa timu ya Katiba na Sheria, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo Ofisi ya Makamu wa Rais ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais Kamba wanawake, wakishangilia ushindi wa chee waliopata baada ya wapinzani wao Katiba na Sheria kuingia mitini.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Kamba na Soka, wakiwa katika picha ya pamoja, baada ya timu zao za Kamba (KE) na (ME) kushinda katika michezo yao.
Kamba wananwake Bunge na Uchukuzi, wakiburuzana. Katika mechi hii, Bunge walishinda baada ya kuwaburuza wenzao mara mbili mfululizo.
'RAHA YA USHINDI BAO', Wachezaji wa timu ya Kamba ya Habari, wanaume wakishangilia ushindi wao baada ya kuwaburuza mara mbili mfululizo wapinzani wao, Uhamiaji katika mchezo wao uliochezwa leo asubuhi, kwenye viwanja vya Chuo Kikuu UDOM, mjini Dodoma.
Wachezaji wa timu ya Habari (kushoto), Kamba wakionyeshana umwamba wapinzani wao wa timu ya Uhamiaji, wakati wa mchezo wao uliochezwa leo asubuhi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM mjini Dodoma. Katika mchezo huo Habari ilishinda kwa raundi mbili mfululizo.
Mchezaji wa timu ya wanawake Kamba ya Uhamiaji, akibebwa kuwekwa pembeni ili kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka wakati walipoburuzwa na wenzao wa Habari na kuwavuta mara mbili mfululizo, katika mchezo wao uliochezwa kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM leo asubuhi.
Uhamiaji wanawake wakijaribu kugangamala kuwazuia Habari, lakini waliburuzwa katia mechi hiyo.
*****************************************
Na www.sufianimafoto.com
TIMU ya Kamba ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Wanawake leo imeibuka na ushindi wa mezani baada ya timu ya kamba wanawake ya Katiba na Sheria kuingia mitini.
Mwamuzi wa mchezo huo alipuliza kipyenga na kutoa ushindi huo kwa timu hiyo ya Ofisi ya Makamu wa Rais, wanawake baada ya kuita timu zote kuingia uwanjani kwa ajili ya kucheza na kujitokeza timu moja ambayo ilipewa ushindi wa bure. Kwa ushindi huo sasa timu hiyo ya Wanawake OMR, inatarajia kucheza na timu ya Bunge kesho katika viwanja vya Chuo Kikuu UDOM.
Wakati wanawake wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakipata ushindi wa chee, wenzao wanaume pia wameshinda mchezo huo kwa kuwaburuza bila huruma timu ya Katiba na Sheria wanaume, katika raundi zote mbili mfululizo.
Timu ya Soka ya Ofisi ya Makamu wa Rais inashuka dimbani leo mchana saa nane kutupa karata yake ya kwanza kwa kukipiga na Mambo ya nje, mchezo utakaochezwa kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma.
Akizungumza na mtandao huu, Kocha wa timu hiyo, Ucheche, alisema kuwa amekiandaa kikosi chake chenye wachezaji wazoefu waliojipanga kuonyesha soka la ukweli jioni ya leo.
Aidha aliwataja baadhi ya wachezaji wanaokiwakilisha kikosi chake kuwa ni pamoja na Jumanne, Mhina, Kihoko, Issa, Sufiani, Lucas, Kifaru, Mandia, Kibik, Mascat na wengineo.
0 comments:
Post a Comment