BAO
pekee la kiungo Salum Abdul Telela jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
limeipa Yanga SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC na kutwaa Ngao ya Jamii.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Oden Mbaga, aliyesaidiwa na Hamisi
Chang’walu na Omar Kambangwa wote wa Dar es Salaam, hadi mapumziko Yanga SC
walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Yanga ilipata bao hilo mapema tu dakika ya pili, mfungaji kiungo Salum Abdula
Telela aliyeunganisha pasi ya Didier Kavumbangu.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea kucheza
vizuri na kukosa mabao zaidi, huku sifa zaidi akistahili kipa chipukizi Aishi
Manula.
Dakika ya 67 Telela alikarbia kufunga tena baada ya
kuunganishia nje krosi nzuri ya Haruna Niyonzima.
Dakika ya 81 Niyonzima alikaribia kufunga mwenyewe
kwa mpira wa adhabu, lakini shuti lake liligonga mwamba wa juu na kudondokea
chini kabla ya beki Aggrey Morris kuondosha katika hatari.
Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa;
Ally Mustafa ‘Barthez’/Deo Munishi ‘Dida’ dk15, Juma Abdul, David Luhende,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Mbuyu Twite dk15, Athumani Iddi ‘Chuji’,
Simon Msuva, Salum Telela, Jerry Tegete/Hussein Javu68, Didier Kavumbangu na
Haruna Niyonzima.
Azam FC; Aishi Manula, Erasto
Nyoni/Joackins Atudo dk46, Waziri Salum, David Mwantika, Aggrey Morris, Himid
Mao, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Gaudence
Mwaikimba dk74, Kipre Balou/Ibrahim Mwaipopo dk62 na Khamis Mcha. SOURCE: BIN ZUBERI BLOG.
|
0 comments:
Post a Comment