Serikali
imeanzisha mkakati wa kutokomeza wimbi la tatizo la dawa za kulevya
nchini kwa kudhibiti viwanja vya ndege na
sehemu mbalimbali za mipakani
zinazotuhumiwa kupitisha dawa za kulevya.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye
ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Assah Mwambene (pichani juu) leo jijini Dar es
salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara
hiyo.
“Kwa yeyote aliyekuwa anafikiria kufanya
biashara ya dawa za kulevya ajue muda wake umekwisha” alisema Mwambene.
Mwambene alisema kuwa tatizo hili litakuwa
historia kwani ulinzi umeimarishwa,
hivyo ametoa rai kwa mtu yeyote mwenye nia ya kufanya biashara hiyo aache mara moja.
Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa Serikali
imeweka jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa watumiaji na waathirika wa dawa za
kuelevya ili waweze kubadili tabia zao za kutumia dawa hizo na kuwa watu wema
katika jamii.
Aidha Mkurugenzi Mwambene amekanusha taarifa
zilizoandikwa kwenye mtandao wa “twitter” kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda
Juvenal Havyarimana.
“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka
matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete”, ameongeza Mwambene.
Assah Mwambene amefafanua kuwa lengo la mitandao
ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha Umma na si kupotosha jamii kwa kuandika
habari zisizo na ukweli wowote. Ameripoti Eleuteri Mangi – MAELEZO.
0 comments:
Post a Comment