Jamali
Ngoma
wa timu ya Flamingo Klab akicheza dhidi ya timu ya Yakwetu Klab wakati
wa ufunguzi wa
mashindano ya Pool Taifa ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Pwani yaliyofanyika
kwenye Baa ya Kontena
Kibaha Maili moja, Mashindano haya yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania(TBL) kupitia Bia ya Safari Lager yakijulikana kwa Safari
National Pool Competition 2013.
Syakyala Mwansasu wa timu ya
Flamingo akichecheza wakati ufunguzi huo.
Yakob Msando wa timu ya Kontena
akimalizia mpira mweusi wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo dhidi ya Klabu ya Kiluvya B.
Na mwandishi wetu,Kibaha
Mikoa iliyoanza mashindano ya Safari Pool Taifa wiki hii ni
Pwani,Lindi,Mwanza Mara,Arusha ,Tanga ,Manyara,Temeke ,Ilala na
Kinondoni.
Mikoa ambayo tunatarajia itapata mabingwa watakaowakilisha mikoa hii
ambao ni vilabu ni Pwani,Lindi Mwanza,Mara,Arusha,Tanda,na manyara
ambapo mashindano haya yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii
jumapili.
Mikoa ambayo tayari ilmeshapata mabingwa watakao wakilisha mikoa yao
katika mashindano ya kitaifa Mkoani Morogoro Augusti 19 mpka 22 ni
Shinyanga,Tabora,Kagera na Kilimanjaro.
Baada ya hapa kutakuwa na mapumziko ya mwezi mmoja kwa mfungo wa Ramadhani na baadae mashindano yataendelea kwa mikoa iliyobaki
Baada ya hapa kutakuwa na mapumziko ya mwezi mmoja kwa mfungo wa Ramadhani na baadae mashindano yataendelea kwa mikoa iliyobaki
0 comments:
Post a Comment