Wananchi waliofurika katika
Tamasha la Filamu la Grand Malt linalofanyika katika Uwanja wa Nyamagana,
Mwanza wakifuatilia mambo yanavyoendelea.
MWANZO MWISHO! Leo ni leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa, wakati kutakapofungwa rasmi Tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima.
Huku wasanii wote mashuhuri wa filamu wakitarajiwa pia kufanya vitu vyao jukwaani, kazi kubwa itakuwa kwa burudani kali zitakazotolewa wakati wa kufunga tamasha hilo.
Mbali na hilo, pia
kutakuwa na shindano kali hatua ya fainali ya kusaka wakali wa kurap pamoja na
kukata nyonga, ambao nao watajiondokea na kitita kikubwa cha fedha.
Akizungumzia hilo, Mratibu
wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema kutakuwa na mambo makubwa zaidi uwanjani
hapo na kuwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia kile
kitakachoendelea.
“Kila kitu kipo tayari na
wasanii wote wakali wa filamu watakuwepo ili kutoa burudani kwa mashabiki
waliofika hapa, huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa,” alisema.
Baadhi ya wasanii wa
filamu wanaotarajiwa kuwepo ni Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Vicent Kigosi
‘Ray’, Shamsa Ford, Ritchie Ritchie, Steven Jacob ‘JB’, Chuchu Hans, Steve
Nyerere, Hashim Kambi na wengineo wengi.
Akizungumzia hilo, Meneja
wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, amefurahi kuona tamasha hilo
limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, huku akitaka mashabiki kufurika Nyamagana leo
kuona kile kinachoendelea.
“Hapa Mwanza tumeshuhudia
vipaji vya kila aina, nimefurahi kwa kiasi kikubwa kuona mashabiki
walivyolipokea tamasha hili, kwetu Grand Malt tunaamini lengo letu limefanikiwa
kwa kiasi kikubwa,” alisema.
Katika mashindano ya kurap
na kucheza katika kila eneo mshindi wa kwanza anatarajiwa kuondoka na Sh
200,000 wa pili Sh 100,000 na watatu Sh 50,000.
Tamasha la Filamu la Grand
Malt lilianza rasmi mwishoni mwa wiki na linatarajiwa kumalizika leo, huku
wakati wote wa tamasha hilo zikionyeshwa filamu mbalimbali za Tanzania.
Tamasha hilo la filamu
limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa
na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
0 comments:
Post a Comment