MWILI wa mwandishi mkongwe David Michael Majebelle. aliyefariki alfajiri ya Jumapili iliyopita unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam Julai 18
Kwa mujibu
wa taarifa rasmi ya familia iliyotolewa leo, mwili huo utaletwa kutoka
katika hospilai ya Mwananyamala ulikohifadhiwa kisha kupelekwa
nyumbani kwake eneo la Sinza jirani na Lion Hotel ambapo heshima
za mwisho zitatolewa majira ya saa sita mchana kisha kulepekekwa katika
kanisa katoliki la Maria Mama wa Mwokozi lililopo Sinza na baadaye saa
tisa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni.
Marehemu
Majebele alizaliwa tarehe 03/05/1941 katika kijiji cha Ibiri, Wilaya ya
Tabora Vijijini, Mkoa wa Tabora, akiwa mtoto wa tatu (3) wa familia ya
watoto 10 wa Mzee Michael Kanyata Majebelle na Mama Theresia Malwa
Majebelle ambao wote kwa sasa ni marehemu.
SHULE
Alisoma
shule ya Msingi ya Bukene (1950) Puge, Wilaya ya Nzega, Mkoa wa Tabora
tangu mwaka 1951, Baadaye katika Shule ya Kati (Middle School) ya
Sikonge, Wilaya ya Sikonge, Mkoa wa Tabora, mwaka 1954 mpaka 1957.
Alijiunga na Tabora Boys School kwa masomo ya sekondari mwaka 1958 mpaka mwaka wa 1961.
Marehemu alikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na aliwahi kushiriki kwenye mashindano ya SUNLIGHT CUP enzi zake.
KAZI
David
aliajiriwa na kampuni ya Almasi ya Williamson Diamonds Ltd ya Mwadui,
Shinyanga mwaka 1962 kama Public Relations Trainee. Mwaka 1963
alipelekwa Uingereza kusomea Stashahada ya Uandishi wa Habari/Upigaji
Picha za Uandishi.
Baada
ya kuhitimu alibaki nchini humo kwenye Kampuni ya The Anglo American
Corporation kupata uzoefu kable ya kurejea Mwadui kuendelea na kazi ya
Afisa Uhusiano wa kampuni ya Williamson Diamonds Ltd hadi Septemba 1967
alipojiuzulu na kuajiriwa na Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East
African Airways) na kituo chake cha kwanza kikiwa ni Uwanja wa Kimataifa
wa Embakasi – Nairobi. Oktoba 1971 alipewa uhamisho na kupelekwa London
Uingereza kuwa mwakilishi wa Shirika hilo kwenye uwanja wa Ndege wa
Kimataifa HEATHROW – London.
Julai
1974 alihamishwa kutoka Uingereza na kuletwa Tanzania kuwa Meneja Mauzo
wa Kampuni Tanzu ya Shirika lililojulikana kwa jina la SIMBA AIR.
Lilipovunjika Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African
Airways)’
David
Majebelle alijiunga na Shirika jipya la Ndege la Tanzania (Air
Tanzania) kama Meneja Mauzo. Mwaka 1978 aliacha kazi katika Shirika hilo
na kujiunga na wamiliki wa magazeti ya AFRICA NEWS na baadaye NEW
AFRICA mpaka mwaka wa 1990 kituo chake kikiwa Uingereza. Baada ya pale
alianzisha Kampuni yake binafsi kwa jina la MEDIA ADVERTISING CO.Ltd
iliyojihusisha na Uhusiano, Matangazo, Upigaji Picha ikiwemo za magazeti
mbalimbali kama;
The Financial Times of London, New Africa African Business, Profit Magazine ,The African Review na magazeti ya hapa nyumbani
Kadri
umri wake ulivyokwenda aliandamwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo
la damu. Ilibidi apunguze kasi ya kushughulikia Kampuni hiyo mpaka
alipoifunga.
FAMILIA
David Michael Majebelle alifunga ndoa mwaka 1975. ameacha mke na watoto wane (4), wa kiume mmoja na wa kike watatu.
UMAUTI
Katika
miaka miwili ya mwisho wa maisha yake, marehemu amekuwa akisumbuliwa na
kisukari na shinikizo la damu. Jumatano iliyopita alifanyiwa vipimo
huko hospitali ya Agha Khan ambako aligundulika kuwa amepata “multiple
mild strokes”. Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita alifariki dunia.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.
Raha ya milele umpe ee Bwana; na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina.
0 comments:
Post a Comment