Nafasi Ya Matangazo

July 22, 2013


Maharusi Dk. Thomas Lujuo na Nuru Lwambano wakiwa ni wenye furaha dakika chache baada ya kuvishana pete za ndoa katika Kanisa Katoliki Parokia ya St. Peters Oysterbay, jijini Dar es Salaam. Ndoa hiyo ilifungwa Julai 20, 2013 na Paroko Msaidizi wa Kanisa Hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tumaini Media, Father. Paulo Haulo na baade maharusi hao waliungana n wanafamilia katika tafrija iliyofanyika Mwika Hall Sinza. 

Production: MD Digital Company:- Mob: +255 373 999; +255 717002303 Whatsapp: +255 788 207274.


 Bi Harusi akiwa na msimamizi wake kabla ya kwenda kanisani.
 Maharusi wakisubiri kufungishwa ndoa yao takatifu.
 Wasimamizi wakiwa kanisani
 Wazazi pamoja na ndugu jamaa na marafiki wakiwa kanisani
 Ndugu Jamaa na marafiki wakiwa Kanisani wakati wa Ibada ya Ndoa
 Nuru akimvisha Pete Mumewe Dk. Thomas
 Father Paulo Haule akimpa Sakrament Bi Harusi Nuru.
 Father Paulo Haule akimlisha Sakrament takatifu Dk. Thomas
 Wanakwaya wakiwa Kanisani wakiimba wakati wa Ibada ya Ndoa.
  Maharusi wakuiweka saini vyeti vyao vya ndoa.
 Jamani tumehitimu urafiki, uchumba na sasa ni WANANDOA... na hivi ndio vyeti vyeti vya kuthibitisha hilo.
 Wapambe wakiingia ukumbi wa Mwika Sinza Makaburini tayari kwa kuanza tafrija.
 Maharusi hao nao wakiingia ukumbini
 Wanafamilia walijipanga kuwapokea kwa shangwe.
 Picha ya pamoja ya Kamati ya Maandalizi.
 Mwenyekiti wa Kamati akikabidhi zawadi ambayo ni Stakabadhi ya kuweka hela Benki zaidi ya Milioni 2.
 Wakisubiri maelekezo ya MC wa Shughuli hiyo Godwin Gondwe
 Bwana Harusi Dk. Thomas akitambulisha mkewe na familia yake kwa ujumla.
 Bi Harusi Nuru akitambulisha familia yake
 Maharusi wakikata keki
 Ulishanaji wa keki ulikuwa ni wa staili yao. Na licha ya kuwa Bi harusi alikuwa mfupi lakini zoezi lilipendeza sana.
 Dk. Thomas akikabidhi keki kwa wakwe zake...
 Ni heshima tu na hakuna la ziada... Bi harusi Nuru akikabidhi keki kwa wakwe zake.
 Mvinyo wa kupongezana ulifunguliwa na Kanali Mstaafu wa Jeshi.
..... Mungu atutangulie katika ndoa yetu hii
 heri na fanaka ilitoka kila kona
 Watu weeeeeeeee.... dada huyo ameolewa dada huyo...ameolewa...
 Mpango mzima na hii ndio sherehe ya ndoa
 Maharusi wakiweka salio la uhai sawa.
 Ilikuwa ni furaha hadi raha kwa maharusi.
 Zawadi na Pongezi zilitolewa kwa maharusi.
 Wazazi nao walitoa pongezi
 Wazazi walipewa zawadi kwa malezi mema...
Hapo sasa... hii ngoma we acha tu KWAITO ilipigwa vilivyo...
Posted by MROKI On Monday, July 22, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo