
Ilikuwa ni simanzi kwawale hasa waliokuwa wakipata Burudani kutoka kwa Albert Mangwair na hakika aliyethibitisha kwa kuona kuwa sasa amelala na hainuki hadi Masiha atakapo rudi walishindwa kujizuia kwa vilio kama Rasta huyu kutoka Ukonga Mazizini maarufu kwajina la Simaga akitokwa na machozi baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mamia ya Wakazi wa jiji walijitokeza kumuaga Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya aliyefariki Mei 28, mwaka huu Nchini Afrika Kusini alikokuwa kwa shughuli za kimuziki.
Mangwewa alisafirishwa mchana wa leo kwenda Kihonda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayo fanyika kesho.









Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Ngwair ikiwa jukwaani.
0 comments:
Post a Comment