Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim
“Uncle” Lundenga akisisitiza jambo na kwa warembo wa Redds Miss Sinza
2013 alipotembelea kambi ya mazoezi hayo. Warembo hao watapanda jukwaani
Ijumaa kuwania taji la mwaka huu.
**** *****
Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa kampuni ya
Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga amewafagilia warembo 12
wanaowania taji la Redds Miss Sinza 2013 kuwa kila mmoja anaweza kutwaa taji
hilo katika mashindano yaliyopangwa kufanyika kesho Ijumaa kwenye ukumbi wa
Meeda Club uliopo Sinza Mori.
Lundenga alisema hayo
katika hotuba yake fupi baada ya kutembelea kambi hiyo akiwa na kamati yake
yote ya Redds Miss Tanzania. Wajumbe wengine waliokuwepo katika msafara huo ni
Bosco “Mshua” Majaliwa ambaye ni Katibu Mkuu, Albert Makoye (Mkuu wa Itifaki),
Hidan Ricco (Afisa Uhusiano) na Yason Mashaka.
Alisema kuwa warembo wa
Redds Miss Sinza wanakazi kubwa ya kulinda heshima ya mwaka jana ambapo
Brigitte Alfred alitwaa taji hilona baadaye kutwaa taji la Miss Kinondoni na
Tanzania.
“Mpo vizuri na
ninatarajia kuona ushindai mkubwa, naamini majaji watafanya kazi kubwa na
mshindi atakayepatikana atakuwa wa halali, kwani hakuna upendeleo katika
kutafuta mshindi, mara nyingi tumekuwa tukitafuta mrembo bora na si bora
mrembo,” alisema Lundenga.
Alisema kuwa warembo
wote 12 wanatakiwa kujua uwa hakuna rushwa ya ngono katika mashindano hayo na
wale wanaosema hivyo wana lengo la kuharibu sifa ya mashindano hayo.
Aliongeza kuwa mshindano hayo yana miaka 20
sasa na washindi wamepatikana kwa njia ya halali na kama kuna masuala ya ngon
basi hiyo ni tabia ya msichana na wala hayahusiani na mashindano.
Mratibu wa mashindano
hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi yamekamilika nay a Twanga Pepeta
itatumbuiza siku hiyo huku ikitambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya zilizomo
katika albamu ya 12 ijulikanayo kwa jina la Nyumbani ni Nyumbani.
“Ikukmbukwe kuwa twanga
pepeta haijatumbuiza Sinza kwa kipindi kirefu na hivyo kuandaa zawadi maalum
kwa mashabiki wake katika mashindano hayo yaliyo dhaminiwa na Redds Original,
Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Fredito Entertainment, CXC Africa,
Clouds Media Group, Salut5.com na Sufiani Mafoto blog,” alisema Majuto.
Wakati huo huo, mbunifu
wa mitindo, Veronica Lugenzi atawavalisha nguo warembo hao watakaopanda
jukwaani kesho, Veronica ambaye alimvalisha nguo Miss Universe Tanzania wa
mwaka jana, amechukua jukumu hilo baada ya kuvutiwa na ubora wa warembo hao.
0 comments:
Post a Comment