Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini Timu ya Taifa (Taifa Stars), george Kavishe akisalimiana na Nahodha wa Taifa Stars Juma Kaseja wakati wa hafla fupi ya
kuzungumza na wachezaji jana kabla ya mechi dhidi ya Ivory Coast. Kushoto ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki.
Meneja wa
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayodhamini Timu ya Taifa (Taifa Stars), george Kavishe
akisalimiana na mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu wakati wa hafla
fupi ya kuzungumza na wachezaji jana kabla ya mechi dhidi ya Ivory Coast.
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe
(kulia) akiteta na Kocha wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen wakati wa hafla fupi ya
kuzungumza na kikosi cha Taifa Stars kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Ivory
Coast.
***** ******
Wadhamini wa
Timu ya Taifa (Taifa Stars), Kilimanjaro Premium Lager wamewaomba watanzania
washikane na kuungana pamoja wakati wa mechi dhidi ya Ivory Coast kutafuta
tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwani kuna watanzania ambao tayari
wamekata tamaa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George
Kavishe alisema Taifa Stars inatakiwa kuungwa mkono na kushangiliwa kwa nguvu
kwani wachezaji wameonesha kuwa wana uwezo.
“Hawa ni
wanajeshi wetu…nawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi…tuwape sapoti na
tuoneshe uzalendo kwani kwenye mpira lolote linawezekana,” alisema.
Bw Kavishe
alisema watanzania lazima welewa timu hii bado ni changa na ina wachezaji wapya
wenye umri mdogo ambao wameonesha uwezo mkubwa.
“Hata
ikitokea tusifuzu kwenda Kombe la Dunia, vijana wameshaonesha dalili nzuri na tuna
imani tutafanya vizuri katika mashindano mengine kama AFCON na CHAN,” alisema.
Aliwataka
wachezaji kutulia uwanjani na kutobabaishwa na ukubwa wa timu ya Ivory Coast
kwani wana uwezo wa kuwafunga na kushangaza dunia nzima Jumapili.
“Hii ni kama
fainali kwa Ivory Coast na wao pia wamebabaika na kuitilia maanani kabisa mechi
hii kwa sababu tukiwafunga ina maana hawatakuwa na uhakika wa kufuzu katika
hatua inayofuata,” alisema Kavishe.
Bia ya Kilimanjaro
Premium Lager imetimiza mwaka mmoja tangu ianze kuidhamini Taifa Stars na wadau
mbalimbali wamesifia udhamini huu kwani umeleta mabadiliko makubwa katika timu
ya Taifa.
Timu ya
Ivory Coast iliwasili nchini Alhamisi usiku na imeweka kambi katika hoteli ya
Bahari Beach, Kunduchi tayari kwa mechi itakayopigwa katika Uwanja wa Taifa
JUmapili hii saa tisa kamili.
Kwa mujibu
wa TFF maandalizi yote yamekamilika na mechi hii inatarajiwa kuangaliwa na
maelfu ya watanzania watakaojitokeza uwanjani na kupitia runinga pia.
Ivory Coast
inaongoza katika kundi C ikiwa na pointi 10, Tanzania ya tatu na pointi 6,
Morocco ya tatu na pointi 5 na Gambia ni ya nne na pointi 1.
0 comments:
Post a Comment