Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati), Mkurugenzi wa Benki ya Dunia
nchini, Philippe Donger (kushoto) na waziri wa nchi Tamisemi, Hawa
Ghasia(wapili kushoto) na baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi wa mradi
wa kuimarisha halmashauri za miji 18 uliofadhiliwa na benki ya dunia
katika picha ya pamoja jana, manispaa ya moshi mkoani kilimanjaro.
***** *****
Fadhili Athumani, Moshi
WAZIRI
mkuu wa Jamhuri ya Tanzania, Mizengo Peter
Pinda amezindua mradi wa kuimarisha halmashauri za miji 18 ya Dola
milioni 225 inayofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka benki ya dunia.
katika
hafla hiyo iliyofanyika leo, katika ukumbi wa Kuringe, Manispaa ya
Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Waziri Pinda amezitaka Halmashauri zote
kuhakikisha zinajenga tabia ya kutenga Bajeti
kwa ajili ya kutunza miradi yote inayoanzishwa hapa nchini ikiwemo
Barabara na
mradi huo.
Waziri Mkuu Pinda ameyasema hayo katika Warsha ya
uzinduzi wa mradi wa kuimarisha halmashauri zote za miji 18 Tanzania Bara
iliyofanyika jana katika ukumbi wa Kuringe, manispaa ya Moshi, Mkoani
Kilimanjaro, mradi uliofadhiliwa kutokana na Fedha za mkopo wa Dola milioni 225
kutoka benki ya dunia.
Pinda amesema endapo mradi huo unaolenga kuimarisha
Halmashauri ya miji 18 Tanzania bara ya Iringa, Moshi, Tabora, Lindi, Babati,
Kibaha, Geita, Mpanda, Bariadi, Sumbawanga, Shinyanga, Songea, Morogoro,
Singida, Njombe, Musoma, Korogwe na Bukoba itasimamiwa vizuri na kutekelezwa
kwa wakati itawezesha halmashauri kuibua vyanzo vingine vya mapato.
“Mheshimiwa Rais aliagiza na mimi narudia,
Halmashauri zijenge tabia ya kutenga bajeti kwa ajili ya kutumnza miradi
inayoanzishwa ikiwemo barabara na mradi huu tunaouzindua leo,” alisema Pinda.
Pinda amesema uzinduzi wa mradi huo ni thibitisho wa
utayari wa Tanzania kutekeleza kazi kubwa na yenye kuleta matumaini ya maisha
bora kwa wananchi wote na faraja kwa wageni watakaotembelea miji ya Tanzania
siku zijazo.
Pinda ameishukuru Benki kuu ya dunia kwa kuiteua
Tanzania kwa ajili ya mradi huo ambao utekelezaji barani aferika unaanzia
nchini hapa kama mradi wa mfano huku akiwaagiza viongozi wote wa Halmashauri
zote kumi na nane, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuhakikisha mradi huo
unafanikiwa .
“Wote tumesikia kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza
katika Bara la Afrika kuteuliwa kufanya majaribio ya mfumo huu wa kupima
matokeo ya mradi. Uteuzi huu umekuja wakati muafaka ambapo nchi yetu inaonesha
imani kubwa ya jinsi serikali ilivyoamua kuwaletea maendeleo wananchi wake,”
alisema
Waziri Pinda amesema kuwa katika utekelezaji wa
mradi huo, serikali haitafumbia macho uzembe au uharibifu wa fedha na vifaa
utakaosababisha kazi hiyo kukwama na utekelezaji wa chini ya kiwango.
“Mafaniko ya mradi huu yataongeza imani kwa wananchi
wetu, kuvutia wadau wengine kushirikiana na Halmashauri zetu kutekeleza miradi
ya maendeleo, hatufumbia macho uzembe au uharibifu wa fedha au vifaa
utakaosababisha uteklezaji wa mradi huu kukwama,” alisema Pinda.
Awali akisoma taarifa ya wizara, Kaimu Katibu mkuu,
ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI), jumanne Sagini alisema Mradi huo uliofadhiliwa
kwa kiasi kikubwa na Benki ya dunia, unalenga kuimarisha uwezo wa halmashauri
za miji 18 katika utoaji huduma (Urban Local Government strengthening
programme-ULGSP).
Amesema
katika kutekeleza mradi huo, miji yote itakuwa imenufaika pakubwa na hivyo
kubadilisha sura ya miji yetu na kuifanya ivutie uwekezaji, kuishi na kufanya
kazi.
Kwa upande wake waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu
(TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema mradi huo unalenga kuendelea kuziimarisha
halmashauri za miji katika maeneo makuu matano ambayo ni Uboreshaji wa mfumo wa
Mipangomiji, Ukusanyaji wa mapato ya ndani hususan mapato yatokanayo na kodi ya
majengo.
Maeneo mengine yatakayolengwa na mradi huo ni
uboreshaji wa mifumo ya udhibiti wa fedha, manunuzi ya mswala ya mazingira na
kijamii, uboreshaji wa mifumo ya utekelezaji, uendeshaji na utunzaji wa
miundombinu kwa ajili ya huduma za jamii na kuboresha uwajibikaji na uwazi.
Mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano,
kuanzia mwaka 2013 hadi 2018 kwa mkataba kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya
Tanzania, uliosainiwa mwezi desemba mwaka 2012 ambapo jumla ya Dola za
kimarekani milioni 225 zimetengwa huku dola milioni 201 zitapelekwa moja kwa
moja kwenye halmashauri.
0 comments:
Post a Comment