Nafasi Ya Matangazo

June 18, 2013

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (Hayupo pichani)mafunzo hayo ni maalum kwa wakufunzi wa Vyuo vya ufundi na Taasisi za Teknolojia kutoka Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Morogoro na Zanzibar. Mafunzo hayo ya siku nne yamefunguliwa leo katika Hotel ya Blue Pearly jijini Dar es Salaam yanalenga kukuza uelewa wa kutambua gesi haribifu kwa mazingira.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava akifungua mafunzo kwa wakufunzi wa Vyuo vya ufundi na Taasisi za Teknolojia kutoka Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma na Morogoro. Mafunzo hayo ya siku nne yamefunguliwa leo katika Hotel ya Blue Pearly jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira - Ofisi ya Makamu wa Rais, Dk. Julius Ningu.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava (waliokaa wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
Posted by MROKI On Tuesday, June 18, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo