Kila mwaka Benki ya Barclays inaandaa matembezi ya kuchangisha fedha
yaliyobatizwa kwa jina la Step Ahead Walk. Mchakato huu umekuwa ukiendelea toka
mwaka 2006 na Tanzania walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008
ambapo fedha zilichangishwa na
zilitumika kusaidia matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean
Road.
Tunu Kavishe, Meneja Mawasiliano na Huduma kwa jamii wa Benki ya
Barclays Tanzania amesema tukio hili rasmi itafanyika tarehe 8 juni, 2013
katika hoteli ya Golden Tulip kuanzia saa kumi na mbili ya asubuhi na
litahusisha matemebzi ya hisani ya kilomita tano (5) na kila mtu katika jamii
anakaribishwa kushiriki. Pia mtu yeyote anaweza kuchangia pesa kwa kutumia
namba ya Mpesa au tigo pesa 133133.
Mgeni wetu rasmi atakuwa Mheshimiwa Dr Asha Rose Migiro, Naibu Katibu
Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa.
Naye Erwin Telemans, Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT amesema “msaada huu
ambao CCBRT wanaupokea kutoka Benki ya
Barclays ni wa thamani sana ambapo tunafanya
kazi ili kufikia malengo ya Tanzania ambapo jamii itajiwezesha kupaha
huduma bora na salama hasa kwa walemavu wa viungo na pia itawafikia wakinamama
wote na kuhakikishia usalama wao kwenye
huduma ya afya ya uzazi na watoto
wachanga inafanikiwa.
Mkakati huu wa benki ya Barclays Step Ahead utasaidia pia
katika kukinga mapungufu ya mtindio wa ubongo na fistula hapa Tanzania, na vile
vile kuhakikisha kwamba wale waliopata mapungufu wakati wa kuzaliwa wanapata
matibabu katika sehemu za viungo vyao
haraka iwezekanavyo.
Naye Dr, Festus Ilako Mkurugenzi wa AMREF Tanzania amesema “Msaada na
mkakati huu wa benki ya Barclays Tanzania kwa AMREF ni wa kila wakati, na kwa
pamoja tunaweza tukaibadilisha jamii kutoka ilipo katika masuala ya afya kwa
wakina mama na watoto, hivyo kuitengenezea jamii uelewa na ustadi katika
kusimamia afya njema na kuvunja marudio rudio
ya ufukara katika afya na umaskini. Kampeni hii kutoka benki ya Barclays
ijulikanayo kama Step Ahead itasaidia kuelimisha wakunga na wazalishaji katika
wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na kuwawezesha wakina mama wajawazito kujifungua
katika mikono ya salama ya wafanyakazi waliofuzu katika Nyanja ya afya hivyo
kupunguza uchangiaji wa vifo visivyo lazima na ulemavu wa viungo kwa mama na
watoto chini ya miaka mitano. Ushirika
huu baina ya Barclays na AMREF ni mfumo mpya
ambayo utawezesha jamii kupata ubora na unafuu katika masuala ya kiafya.
Mwaka 2011, Benki ya Barclays na washiriki wake walifanikiwa kuchangisha
shilingi za kitanzania milioni 150 kutokana na
mauzo ya tiketi na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili. Mwaka huu lengo
ni kuchangisha zaidi ya marambili ya shilingi milioni 150 kutoka kwenye matoleo
ya washirika muhimu na washiriki wengine katika jamii.
Fedha zitakazochangishwa mwaka huu zitakwenda kusaidia katika masuala ya
uzazi na afya ya watoto kama ifuatavyo:-
1. Mafunzo kwa wakunga wa uzazi
2. Matibabu ya Fistula
3.Upasuaji kwa watoto waliozaliwa
na ulemavu unaosababishwa na uzazi
Step Ahead Walk 2013 itaweza kufanikiwa tu kama itawezeshwa na kila
mshiriki na jamii nzima ya kitanzania kwa ujumla. Kwa sababu hiyo basi tujiunge
wote ili tuweze kufanya badiliko katika masuala ya afya kwa ujumla hapa
Tanzania hususani masuala ya uzazi na afya ya watoto.
Matembezi haya yamedhaminiwa na Montage Ltd, ITV/Radio One Ltd, Clouds
Media group, Mwananchi Communications, Cocacola, NSSF, African Medical
Investments, Home Shopping Centre, Golden Tulip Hotels, Grand Malt na Serena
Hotels.
0 comments:
Post a Comment