NA BELINDA KWEKA – MAELEZO, DSJ
MWANASHERIA Mkuu wa
Serikali mstaafu, Jaji Mack Bomani ametoa
wito wa kupingwa kwa kura ya maoni kwa wakazi wa Tanzania Visiwani ili kuona
kama wanahitaji mfumo gani wa Muungano kabla ya kuendelea na mchakato wa sasa
wa rasimu ya Katiba mpya .
Akizungumza na waandishi wa
habari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari –MAELEZO , Jaji Mack Bomani alisema
anaipongeza tume ya Jaji Joseph
Warioba kwa kazi nzuri na pia kwa mapendekezo yake juu ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo Jaji
Bomani alitoa historia fupi juu
ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambapo ameeleza kuwa muungano huo
ulipendekezwa na hayati Sheikh Abeid Amani Karume
na hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambao walikutana mara baada ya
Mapinduzi ya Zanzibar Januari, mwaka 1964.
Jaji Bomani aliongeza
hayati
Karume alipendelea nchi mbili
kuungana na kuwa nchi moja , lakini hayati Nyerere alisita
kidogo kwa kuogopa kwamba
ingeonekana Zanzibar imemezwa na Tanganyika na pengine kuleta maasi Zanzibar hivyo
kupendekeza kuundwa mfumo wa muda mfupi wakati mfumo wa kudumu ukifanyiwa kazi.
“Suala la
Muungano ndilo suala kubwa kuliko yote katika mchakato
wa Katiba mpya. Niliwahi kuto
ushauri nao ni kwamba ifanyike kura ya maoni ya wananchi hasa Zanzibar kama wanautaka muungano au la na kama
wanautaka uwe muungano wa mfumo gani ?
Mpaka sasa maoni ambayo yanasikika ni maoni ya viongozi mara Zanzibar ijitoe
kwenye muungano mara tuwe na muungano wa mkataba,” alisema Jaji Bomani.
Akijibu maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari ,Jaji Mack Bomani
amesema katika uundwaji wa Serikali tatu anaamini utaweza kumaliza migogoro
inayojitokeza mara kwa mara hasa upande wa Zanzibar kuogopa kumezwa.
“Woga wa gharama za
mfumo wa Serikali tatu hauna msingi.Inategemea Serikali hizo unazifanya
vipi.ipo mifano mingi mno duniani ya miungano ya mfumo mbalimbali,”
alisisitiza.
Pia ameongezea kuwa kama kutaundwa Serikali tatu basi iwe Serikali
ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano.
Akiongezea kuhusu katiba mpya amesema “kwa maoni yangu si
lazima kazi hii ya katiba iishe kabla ya 2015, tupate muda wa kutosha ili
tuweze kupata katiba ya kueleweka na kukubalika na kila mtu”.
0 comments:
Post a Comment