Shirikisho
la Muziki Tanzania (Tanzania Music Federation) tunasikitika kutangaza kifo vya
msanii ALBERT MANGWEA kilichotokea Afrika ya Kusini akiwa kwenye
shughuli zake za kimuziki .
Tunawapa
pole Wazazi, ndugu, jamaa na watanzania wote kwa kuondokewa na mwanamuziki huyo
mkongwe wa kizazi kipya, marehemu tutamkumbuka kwa mengi hasa msimamo
aliounesha katika mambo aliyoyaamini, Alikuwa ni mtu mwenye jitihada hata mauti
ilipomkuta alikua kwenye kujitafutia riziki.
Marehemu
alitambulika sana katika tasnia ya muziki kupitia wimbo wa GETO LANGU TU na
baadae alirekodi nyimbo nyingi zilizopendwa na jamii ya watanzania.
Tunawaomba
watanzania wazidi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu, Shirikisho lenu
lipo imara na tunashiriki kikamilifu katika msiba huu tukishirikiana na wadau
mbali mbali.
Tunapenda
kuwatangazia kuwa Shughuli nzima ya mazishi ya mpendwa wetu ALBERT MANGWEA
zitasimamiwa na Familia ya Marehemu, Shirikisho la Muziki kupitia chama cha
Muziki wa kizazi kipya na wadau mbali mbali.
Kwa sasa
tunakamilisha taratibu zote za awali, maandalizi na ratiba mzima itatoka
baadae. Tulifanya kikao na kaka wa marehemu (KENNETH MANGWEA) na
kukubaliana kuwa msiba utakuwa MBEZI BEACH eneo la GOIG kwa sasa tunashirikiana
vyema katika kukamilisha haya.
Kama mambo
yatakwenda sawa, ikiwa ni pamoja na kuuleta mwili wa marehemu tunatarajia kuaga
siku ya Jumamosi na baadae kusafirisha kwa shughuli ya Mazishi huko Morogoro
eneo la Kihonda nyumbani kwa mama yake mzazi MAMA DENISIA MANGWEA.
Tunaomba
tushirikiane sote kwa PAMOJA katika katika kipindi hiki kigumu. Taarifa zaidi
tutawapatia baadae kadri itakavyo bidi.
Bwana
ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana Lihimidiwe.Vile vile tunampa pole
mwanamuziki Mgaza Pembe (M TO THE P) na kuomba maombi ya watanzania kumuombea
mwanamuziki huyo ambaye aliyekuwa Afrika Kusini na Marehemu. M TO
THE P amelazwa Afrika Kusini.
Tunamuombea apone haraka.
Addo November Mwasongwe (Pichani juu)
Raisi Shirikisho la Muziki
Tanzania
0713396367/0754396367
29th May 2013.
0 comments:
Post a Comment