Nafasi Ya Matangazo

May 31, 2013

Naibu Katibu Mkuu wa baraza la Taifa la Mitihani, Dk. Charles E. Msonde akisoma matokeo hayo ya mitihani ya kidato cha sita kwa mitihani iliyofanyika mwaka huu nchini kote.  

TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA (ACSEE) ULIOFANYIKA FEBRUARI 2013


UTANGULIZI
Baraza la Mitihani la Tanzania katika kikao chake cha 94  kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2013 liliidhinisha kutangazwa rasmi kwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika tarehe 11 - 27 Februari 2013.

USAJILI NA MAHUDHURIO

Watahiniwa wote
Jumla ya watahiniwa 52,513 waliandikishwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2013 wakiwemo wasichana 16,934 (32.25%) na  wavulana 35,579 (67.75%).  Kati ya watahiniwa 52,513 waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita Februari 2013, watahiniwa 50,611 sawa na asilimia 96.38 walifanya mtihani na watahiniwa 1,902 sawa na asilimia 3.62 hawakufanya mtihani.

Watahiniwa wa Shule
Kwa Watahiniwa wa Shule, kati ya watahiniwa 43,231 waliosajiliwa, watahiniwa 42,952 sawa na asilimia 99.35 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa ni 13,883 (99.54%) na wavulana ni 29,069 (99.27%). Watahiniwa 279 (0.65%) hawakufanya mtihani.

Watahiniwa wa Kujitegemea
Kwa upande wa Watahiniwa wa Kujitegemea, kati ya watahiniwa 9,282 waliosajiliwa, watahiniwa 7,659 sawa na asilimia 82.51 walifanya mtihani na watahiniwa 1,623 sawa na asilimia 17.49 hawakufanya mtihani.


MATOKEO YA MTIHANI

Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 44,366 sawa na asilimia 87.85 ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Sita 2013 wamefaulu. Wasichana waliofaulu  ni  14,622 sawa na asilimia 89.19 wakati wavulana waliofaulu ni 29,744 sawa na asilimia 87.21.
Mwaka 2012 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 46,658 sawa na asilimia 87.65.
Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 40,242 sawa na asilimia 93.92 ya waliofanya mtihani.  Wasichana waliofaulu ni 13,286 sawa na asilimia 95.80 na wavulana ni 26,956 sawa na asilimia 93.03.
Mwaka 2012 Watahiniwa 40,775 sawa na asilimia 92.30 ya Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo.

Watahiniwa wa Kujitegemea

Idadi ya Watahiniwa wa Kujitegemea waliofaulu mtihani ni 4,124 sawa na asilimia 53.87.  Mwaka 2012 Watahiniwa wa Kujitegemea 5,883 sawa na asilimia 64.96 walifaulu mtihani huo.

UBORA WA UFAULU

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata Watahiniwa wa Shule unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 35,880 sawa na asilimia 83.74 wamefaulu katika madaraja I - III wakiwemo wasichana 12,108 sawa na asilimia 87.30 na wavulana 23,772 sawa na asilimia 82.04.

Jedwali la 1 linaonesha ufaulu kwa kila Daraja kwa Watahiniwa wa Shule na kwa Jinsi:

Jedwali la 1: Ufaulu wa kila Daraja kwa Watahiniwa Wa Shule

Daraja la Ufaulu
Wavulana
Wasichana
Jumla
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
Idadi
Asilimia
I
188
0.65
137
0.99
325
0.76
II
3,142
10.84
2,230
16.08
5,372
12.54
III
20,442
70.55
9,741
70.24
30,183
70.45
IV
3,184
10.99
1,178
8.49
4,362
10.18
0
2,021
6.97
583
4.20
2,604
6.08


UFAULU WA MASOMO KWA WATAHINIWA WA SHULE

Ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule unaonesha kwamba kwa masomo ya History, Geography, English Language, Chemistry, Biology, Agriculture, Computer Science, Economics na  Accountancy  yamefanyika vizuri zaidi ukilinganisha na mwaka 2012.

Jedwali la 2 linaonesha idadi ya watahiniwa wa shule waliofaulu masomo mbalimbali kwa mwaka 2012 na mwaka 2013.

Jedwali la 2: Ulinganifu wa ufaulu kwa masomo kwa mwaka 2013 na 2012
NA.
MASOMO
WALIOFAULU 2012
WALIOFAULU 2013
IDADI
ASILIMIA
IDADI
ASILIMIA
111
GENERAL STUDIES
38,468
87.09
16,507
38.53
112
HISTORY
21,482
92.86
18,987
97.33
113
GEOGRAPHY
21,823
92.40
20,578
96.87
121
KISWAHILI
13,608
97.89
11,840
96.95
122
ENGLISH LANGUAGE
12,903
89.50
11,081
93.61
131
PHYSICS
7,526
70.58
5,788
46.34
132
CHEMISTRY
10,289
71.14
13,809
83.87
133
BIOLOGY
7,338
77.90
9,181
87.05
134
AGRICULTURE
506
92.67
537
98.35
136
COMPUTER SCIENCE
17
43.59
74
80.43
142
ADVANCED MATHEMATICS
7,786
84.44
6,895
69.32
151
ECONOMICS
8,001
90.66
8,173
93.53
152
COMMERCE
1,405
90.41
1,573
88.57
153
ACCOUNTANCY
1,314
84.56
1,660
93.42


SHULE ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI

Ubora wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade Point Average” (GPA) ambapo A = 1,B = 2, C = 3, D = 4, E = 5, S = 6 na F = 7.  Shule zimegawanywa katika makundi mawili kulingana na idadi ya watahiniwa kama ifuatavyo:
Zenye watahiniwa 30 na zaidi (Jumla ni 329);
Zenye watahiniwa pungufu ya 30 (Jumla ni 166).

6.1       Shule kumi (10) bora katika kundi la shule zenye watahiniwa 30 na zaidi

NA
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
MARIAN GIRLS S.S
158
PWANI
2
MZUMBE S.S
125
MOROGORO
3
FEZA BOYS’ S.S
59
DAR ES SALAAM
4
ILBORU S.S
171
ARUSHA
5
KISIMIRI S.S
50
ARUSHA
6
ST.MARY'S MAZINDE JUU S.S
80
TANGA
7
TABORA GIRLS S.S
74
TABORA
8
IGOWOLE S.S
58
IRINGA
9
KIBAHA S. S
184
PWANI
10
KIFUNGILO GIRLS S.S
61
TANGA

6.2       Shule kumi (10) za Mwisho katika kundi la shule zenye watahiniwa 30 na zaidi

NA
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
PEMBA ISLAMIC COLLEGE
67
PEMBA
2
MAZIZINI S.S
127
UNGUJA
3
BARIADI S.S
34
SIMIYU
4
HAMAMNI S.S
174
UNGUJA
5
DUNGA S.S
35
UNGUJA
6
LUMUMBA S.S
292
UNGUJA
7
OSWARD MANG’OMBE S.S
120
MARA
8
GREEN ACRES S.S
87
DAR ES SALAAM
9
HIGH VIEW INTERNATIONAL
34
UNGUJA
10
MWANAKWEREKWE “C” S.S
126
UNGUJA

6.3       Shule kumi (10) bora katika kundi la shule zenye watahiniwa
chini   ya 30

NA
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
PALLOTI GIRLS S.S
26
SINGIDA
2
ST. JAMES SEMINARY
20
KILIMANJARO
3
PARANE S.S
12
KILIMANJARO
4
SANGITI S.S
12
KILIMANJARO
5
ITAMBA S.S
18
NJOMBE
6
MASAMA GIRLS S.S
19
KILIMANJARO
7
KIBARA S.S
11
MARA
8
ST. LUISE MBINGA GIRLS S.S
19
RUVUMA
9
ST. PETER’S SEMINARY
17
MOROGORO
10
PERAMIHO GIRLS S.S
15
RUVUMA

6.4       Shule kumi (10) za Mwisho katika kundi la shule zenye
watahiniwa chini ya 30

NA
JINA LA SHULE
IDADI YA WATAHINIWA
MKOA
1
MBARALI PREPARATORY SCHOOL
21
UNGUJA
2
PHILTER FEDERAL S.S
23
UNGUJA
3
ST.MARY'S S.S
24
DAR ES SALAAM
4
MZIZIMA S.S
12
DAR ES SALAAM
5
HIJRA SEMINARY
28
DODOMA
6
TWEYAMBE S.S
19
KAGERA
7
MPAPA S.S
17
UNGUJA
8
AL-FALAAH MUSLIM
17
UNGUJA
9
PRESBYTERIAN SEMINARY
14
MOROGORO
10
NIANJEMA S.S
16
PWANI

WATAHINIWA WALIOFANYA VIZURI ZAIDI

Watahiniwa waliofanya vizuri zaidi wamepatikana kwa kuangalia GPA kwenye masomo ya “combination” pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata. Masomo ya hiari (optional subjects) hayakujumuishwa katika kuwapanga wanafunzi bora.

Watahiniwa Watano (05) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Sayansi

NA.
JINA
JINSI
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ERASMI  INYANSE
M
ILBORU
ARUSHA
PCM
2
MAIGE R MAJUTO
M
KISIMIRI
ARUSHA
PCM
3
GASPER SINGFRID MUNG'ONG'O
M
FEZA BOYS'
DAR ES SALAAM
PCB
4
GASPER JAMES SETUS
M
ST. JAMES SEMINARY
KILIMANJARO
PCM
5
LUCYLIGHT E MALLYA
F
MARIAN GIRLS
PWANI
PCB

Wasichana  Watano (05) bora kitaifa kwa Masomo  ya Sayansi

NA.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
LUCYLIGHT E MALLYA
MARIAN GIRLS
PWANI
PCB
2
EDNA BARAKA KIBANGO
MSALATO
DODOMA
PCB
3
SARAH SEVERIN KIMARIO
ST.MARY'S MAZINDE JUU
TANGA
PCM
4
VERONICA S MWAMFUPE
MARIAN GIRLS
PWANI
PCM
5
BEATRICE D ISSARA
ST.MARY GORETI
KILIMANJARO
PCM
Wavulana  Watano (05) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Sayansi

NA.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ERASMI  INYANSE
ILBORU
ARUSHA
PCM
2
MAIGE R MAJUTO
KISIMIRI
ARUSHA
PCM
3
GASPER SINGFRID MUNG'ONG'O
FEZA BOYS'
DAR ES SALAAM
PCB
4
GASPER JAMES SETUS
ST. JAMES SEMINARY
KILIMANJARO
PCM
5
CHRISTOPHER L STANSLAUS
MZUMBE
MOROGORO
PCB

Watahiniwa Watano (05) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Biashara

NA.
JINA
JINSI
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ERIC ROBERT MULOGO
M
TUSIIME
DAR ES SALAAM
ECA
2
ALICIA  FILBERT
F
NGANZA
MWANZA
ECA
3
EVART  EDWARD
M
KIBAHA
PWANI
ECA
4
ANNASTAZIA P RENATUS
F
TAMBAZA
DAR ES SALAAM
ECA
5
PETERSON P MEENA
M
MBEZI BEACH
DAR ES SALAAM
ECA

Wasichana    Watano (05) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Biashara

NA.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ALICIA  FILBERT
NGANZA
MWANZA
ECA
2
ANNASTAZIA P RENATUS
TAMBAZA
DAR ES SALAAM
ECA
3
MARY AMOS BUJIKU
ST.ANTHONY'S
DAR ES SALAAM
ECA
4
GETRUDA GHATI PATRICK
BARBRO-JOHANSSON
DAR ES SALAAM
ECA
5
LETICIA PARTSON KAYANGE
WERUWERU
KILIMANJARO
ECA

Wavulana  Watano (05) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Biashara

NA.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ERIC ROBERT MULOGO
TUSIIME
DAR ES SALAAM
ECA
2
EVART  EDWARD
KIBAHA
PWANI
ECA
3
PETERSON P MEENA
MBEZI BEACH
DAR ES SALAAM
ECA
4
FRANK  BUNUMA
KIBAHA
PWANI
ECA
5
ABDALLAH A JUMA
KAZIMA
TABORA
ECA

Watahiniwa Watano (05) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Lugha na Sayansi ya Jamii

NA.
JINA
JINSI
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ASIA IDD MTI
F
BARBRO-JOHANSSON
DAR ES SALAAM
HGE
2
GODLOVE GEOFREY NGOWO
M
MAJENGO
KILIMANJARO
EGM
3
JOHNSON ELIMBIZI MACHA
M
NJOMBE
NJOMBE
EGM
4
HAMISI JOSEPH MWITA
M
ILBORU
ARUSHA
HGL
5
SIA H SANDI
F
MARIAN GIRLS
PWANI
EGM
Wasichana  Watano (05)) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Lugha na Sayansi ya Jamii

NA.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
ASIA IDD MTI
BARBRO-JOHANSSON
DAR ES SALAAM
HGE
2
SIA H SANDI
MARIAN GIRLS
PWANI
EGM
3
JACQUELINE B AGRIPPA
MASAMA GIRLS
KILIMANJARO
HGL
4
DHULFA A KANGUNGU
KOROGWE GIRLS
TANGA
HKL
5
ANGELIKA D CHENGULA
MSALATO
DODOMA
HGL

Wavulana  Watano (05) Bora  kitaifa kwa Masomo  ya Lugha na  Sayansi ya Jamii

NA.
JINA
SHULE
MKOA
MCHEPUO
1
GODLOVE GEOFREY NGOWO
MAJENGO
KILIMANJARO
EGM
2
JOHNSON ELIMBIZI MACHA
NJOMBE
NJOMBE
EGM
3
HAMISI JOSEPH MWITA
ILBORU
ARUSHA
HGL
4
ABUBAKAR HASSANI MSANGULE
SWILLA
MBEYA
HGL
5
ALEX A MKUNDA
KIBITI
PWANI
HKL

MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA

Baraza la Mitihani la Tanzania limezuia kutoa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2013 ya watahiniwa :
89 wa Shule   ambao hawajalipa ada ya Mtihani. Matokeo yao yatatolewa mara watakapolipa ada wanayodaiwa pamoja na faini.

10 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya   kurudia Mtihani wa Kidato cha Sita 2014 kwa masomo waliyoathirika.

17 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote. Watahiniwa husika wamepewa fursa ya   kurudia Mtihani wa Kidato cha sita, 2014.

WATAHINIWA WALIOBAINIKA KUFANYA UDANGANYIFU KATIKA  MITIHANI

Baraza la Mitihani la Tanzania limefuta matokeo yote ya Mtihani ya mtahiniwa mmoja (01) wa shule na watahiniwa watatu (03) wa Kujitegemea waliobainika kufanya udanganyifu katika Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2013.

KUANGALIA MATOKEO YA MITIHANI

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) uliofanyika Februari 2013  yanapatikana katika tovuti zifuatazo:

Dk. Charles E. Msonde
Kny KATIBU MTENDAJI
31/05/2013
Posted by MROKI On Friday, May 31, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo