Nafasi Ya Matangazo

February 09, 2026




Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw.Frederic Van de vyver Mkuu wa Jeune Afrique Media Group, kampuni inayoongoza ya habari ya ki-panafrika yenye makao yake makuu jijini Paris, Ufaransa. 

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, wamejadiliana ni kwa namna gani wanaweza wakafanya kazi pamoja katika fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Bw. Mchechu alimhakikishia Bw. De vyver kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba atapata ushirikiano wa kutosha.

 “Kwa upande wa sekta ya umma utapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Ofisi ya Msajili wa Hazin ana kwa upande wa sekta binafsi utapata ushirikiano kutoka kwa CEOrt,” alisema Bw. Mchechu.

Kwa upande wake Bw. De vyver alieleza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania.

“Lazima tutafute namna bora ya kushirikiana,” alisema.
Posted by MROKI On Monday, February 09, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo