Washindi wa pili wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football Challenge
Francis Wangari(kushoto) na Kepha Kimani(kulia) kutoka Kenya katika
picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha Pan-Africa Guinness
Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.
Washindi wa kwanza wa nusu fainali ya kwanza ya Guiness Football
Challengekutoka Ghana Naab Jonathan Baan(kushoto) na Desmond
Odaano(kulia) katika picha ya pamoja na waendeshaji wa kipindi cha
Pan-Africa Guinness Football Challenge Larry Asego na Mimi Kalinda.
****** *******
Jana
usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV nusu fainali ya kwanza kabisa ya
GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilirushwa hewani na katika runinga Afrika nzima ambapo timu ya Ghana ilionesha ni kwanini ni timu bora ambayo ndiyo imejishindia pesa
nyingi mpaka sasa.
Jonathan
Nabb na Desmond Odaano walionesha uwezo na ujasiri wao walipoibuka washindi zidi ya
wapinzani wao timu kutoka Kenya katika mchezo wa jana. Katika hatua ya pesa
ukutani walifanikiwa kulenga lango namba nne na hivyo kupata dola za kimarekani
12,000 wanazoziongeza katika dola 8,500 walizokuwa nazo awali katika hatua ya
robo fainali.
Wakenya
Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao ni washindi wa pili katika nusu fainali hii
wataungana na Ghana katika fainali.Ingawa waliikosakosa hatua ya ukuta wa pesa
wa Guinness bado wana nafasi ya kuwa
mabingwa katika fainali.
Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guinness football challenge wanaweza kupima maarifa yao
katika soka kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure
kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia
simu ya mkononi.
Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE
kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa
wale wenye umri chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment