Mwanamitindo,
Flaviana Matata (wa pili kulia) akiomba dua katika kaburi la mama yake
Mzazi maeneo ya Igoma mkoani Mwanza katika siku ya kukumbuka ajali ya MV
Bukoba iliyoua watu takribani 1000 Mei 21, 1996. Flaviana mbali na
kukumbuka waliofariki katika ajali hiyo akiwamo mama yake mzazi pia
alikabidhi msaada wa vifaa vya kuokolea maisha kwa Shirika la
Kiserikali la Usafiri wa Maji Mwanza hapo mwaka jana.
***** ******
Mwanamitindo wa kimataifa wa
Tanzania, Flaviana Matata leo atashiriki katika misa maalum ya kuwakumbuka
watanzania waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba mwaka 1996.
Misa hiyo itafanyika kwenye
eneo la makabuli ya kumbukumbu ya MV Bukoba ambapo Flaviana alipoteza mama yake
mzazi na kaka yake katika ajali hiyo.
Mwaka jana, mwanamitindo huyu
kupitia shirika lake la Flaviana Matata Foundation alitoa msaada wa maboya
yaani vyombo vya kuokoa maisha majini (life vests) 500 kwa mawakala wa meli ya
serikali yaani Marine Services Ltd ikiwa ni nja moja ya kujaribu kusaidia
usalama majini.
Mkurugenzi wa kampuni ya
Compass Communications, Maria Sarungi alisema kuwa mbali ya kushiriki katika
misa hiyo, pia mwana mitindo huyo atafanya mazungumzo na wadau mbali mbali
jinsi ya kuendeleza juhudi za kuimarisha usalama majini.
Flaviana alisema kuwa juhudi
zake kubwa kwa hivi sasa ni kuhakikisha kuwa ajali za vyombo vya kwenye maji
zinaepukika na ndiyo maana anapigana huku na kule katika sakata hilo.
Alisema kuwa lengo lake kubwa
ni kuona vyombo vya kuokolea katika kila meli vinapatikana na hasa kwa kutafuta
misaada kwa wadau mbali mbali.
“Suala la usalama majini bado
haujatiliwa mkazo vya kutosha na jamii pamoja na serikali” alieleza
mwanamitindo huyu. “Muda umefika kwa wahusika wote kushirikiana kwa pamoja
kuzungumzia na kukabiliana na changamoto hii” alisema Matata.
0 comments:
Post a Comment