Washindi
wa kipindi cha tano cha Guinness Football Challenge Ken Muturi
(kushuto) na Chis Mwamgi(kulia) wakishangilia ushindi walioupata huku
wakiwa wamebeba pesa taslimu walizojishindia katika shindano hilo jana
usiku na pembeni ni mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho Lary
Asengo(anayepiga makofi kulia).
Washindi
wa kipindi cha Tano cha Guinness Football Challenge, Chris
Mwamgi(kushoto) na Ken Muturi(kulia) katika picha ya pamoja na
watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego and Flavia Tumsiime jana
baada ya ushindi.
****** ******
Jana usiku kupitia Televisheni za ITV na Clouds TV timu ya Tanzania ilishindwa
kutumia nafasi ya kipindi cha mwisho cha mashindano ya “Guinness Football
Challenge” katika hatua ya Afrika Mashariki baada ya kutolewa na timu kutoka
Kenya. Rangi nyekundu imeonekana kuwa ni rangi ya bahati kwa timu za Kenya kwani
hii ni timu ya nne kutoka Kenya kufanikiwa kufuzu kuingia hatua ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGETM.
Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi ndio walioibuka washindi jana usiku kwani walifanikiwa
kufika katika hatua ya mwisho ya kulenga ukuta
wa pesa wa Guinness ambapo walijishindia dola za kimarekani 1,500.
Ni vipi Kenneth na
Chris wataweza kumudu hatua ya Pan-African? Sasa wana nafasi ya kuiwakilisha
nchi yao katika mashindano ya Pan-African ambapo watakutana na wawakilishi
pekee kutoka Tanzania, Daniel Msekwa na Mwalimu, washiriki kutoka Uganda Alex
Muyobo na Ibrahim Kawoova pamoja na wenzao kutoka Kenya,Francis Ngigi na Kepha
Kimani(washindi wa kipindi cha 2), Kenneth Kamau na Wills Ogutu(washindi
kipindi cha 3) na Ephantus Nyambura na Samuel Papa(washindi kipindi cha 4).
Timu hizi tano zitakua
uwanjani kutimiza malengo yao, ambapo watakutana uso kwa uso na washiriki
kutoka Ghana na Cameroun kuonesha ni nani ana maarifa zaidi na ujuzi wa
kusakata kabumbu, hata kuvishwa ubingwa
wa Pan-African na kuondoka na dola za
kimarekani 250,000.
Usikose kuangalia mashindano haya kupitia televisheni za ITV na
Clouds TV huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.
Tafadhali kunywa
kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment