Nafasi Ya Matangazo

April 23, 2013


 Mshindano makubwa na mazuri ya GUINNESS® FOOTBALL™ CHALLENGE yamekuwa yakiwasisimua na kuwafurahisha watazamaji wake kwa wiki tano zilizopita.Sasa mashindano ya Pan-African yataanza kuoneshwa katika televisheni za ITV  na Clouds TV kuanzia kesho tarehe 24 April, 2013 saa 3:15 ITV na 2:15 Clouds TV. Sasa timu kutoka Cameroon, Ghana, Uganda, Kenya na Tanzania zitakutana uso kwa uso kushindana ili kujua ni nani ana maarifa zaidi na ujuzi wa kusakata kabumbu,  hata kuvishwa ubingwa wa Pan-African.

Washiriki kutoka Afrika yote waliowashinda wapinzani zao ili kuwakilisha nchi zao sasa watakutana na timu bora za Pan-African ambazo zina maarifa na ujuzi zaidi. Katika hatua hii ya robo fainali washiriki wanawania kushinda hadi dola za Kimarekeni 250,000.
Kila timu sasa itacheza kuwakilisha nchi yake na kuonesha uwezo wao katika kusakata kabumbu. Washiriki watahitaji kucheza vizuri kwa kiwango cha juu katika mchezo ili kujipa nafasi ya kushinda mashindano haya na kufanya nchi zao kujivunia. Timu nne zitakazo shiriki katika robo fainali ya kipindi cha kwanza ni:       

·         Gregory Doamekpor na Kyei Edmond Nana, wenye umri wa miaka 21 kutoka Accra,Ghana. Hawa walikuwa washindi katika sehemu ya kwanza ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE Ghana. Gregory ni mwanafunzi wa Saikolojia na ndiye kichwa cha timu wakati Kyei ni mwanafunzi wa Mahusiano ya jamii, atakuwa anachezea mpira.

· Timu kutoka Uganda itakuwepo pia, Ibra Kawooya(30) na Alex Muyobo(31),wote mashabiki wa Man.United, Ibra atakuwa kichwa cha timu wakati Alex atacheza uwanjani. ·         Kutoka Cameroon watakuwa Emerand Tchouta(24) na Abdul Salam(25). Emerand atakuwa kichwa cha timu na Abdul ataonesha uwezo wa kusakata kabumbu. Japo walifanikiwa kuondoka na dola 1,500 tu lakini walionesha kiwango kizuri hivyo wana nafasi kubwa ya kushinda. ·         

Timu nyingine kutoka Kenya Francis Ngigi(23) kutoka Nairobi na Kepha Kimani(25) kutoka Thika.Timu hii ilishinda dola 3,000 katika mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE. Francis atakuwa kichwa cha timu wakati Kepha ataonesha kipaji chake cha kucheza soka.

Meneja wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi alisema: “Tumeona timu mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali zilishindana kufikia hatua ya robo fainali ya Pan-African- GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE na sasa tunafurahia kuona timu zetu bora katika hatua za mwisho. Kila timu imeiwakilisha vizuri nchi yake na wamefanya vizuri katika mashindano haya kwa kujiamini. Sasa timu zote zina nafasi ya kuthibitisha uwezo wao wa kucheza na si kuangalia tu pale watakapo shindana ili kufikia nusu fainali.Tunasubiri kwa hamu na kuzitakia timu zote kila la heri!”

Robo fainali ya kwanza ya Pan-African itaoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV  kwa hiyo hakikisha unaangalia na kuishangilia timu ya taifa lako. Wapenzi wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu.   Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili  bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.  

Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
Posted by MROKI On Tuesday, April 23, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo