Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata,
Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph
Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha na
mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri
zaidi.
“Warembo wazuri wamejitokeza zaidi
kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi
kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen
Arts.
Warembo watakaoshiriki kwenye
shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West
Park.Warembo hao ni Pendo Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma
Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19), Upendo Dickson Lema (22), Martha
Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19),
Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja
(19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20),
Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Wengine ni Lilian Mpakani (19),
Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rafhel Mussa (19),
Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis
(19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass
(22).
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa
kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la
Kanda ya Ilala.
"Bado milango iko wazi, mrembo
yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka
huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza. Warembo 10 watachaguliwa
kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa
sasa Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala. Waliyojitokeza kudhamini
shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5
0 comments:
Post a Comment