Na
Mwandidhi wa EANA
Rais
mpya wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesisitiza kuendeleza ushirikiano katika Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) kwani amesema ni moja ya nguzo muhimu katika kipindi
cha utawala wake.
''Lengo letu kuu
katika kuimarisha biashara na uwekezaji utakuwa ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki
na Afrika kwa ujumla,'' Rais Kenyatta alinukuliwa akisema alipokutana na Katibu
Mkuu wa EAC, Dk Richard Sezibera aliyekwenda kumtembelea ofisini kwake mjini
Nairobi Juzi.
Aliongeza
kuwa kuondolewa kwa vikwazo vya biashara kupewe kipaumbele kadiri mtangamano wa
EAC unavyozidi kuimarika na kupanuka, Shirikia Huru la Habari la Afrika
Mashariki (EANA) limeripoti.
''Kuondolewa
kwa vikwazo vya kazi na kusafiri kwa raia ndani ya nchi wanachama kutasaidia
zaidi kukua kwa biashara na kubadilishana mawazo,'' alisema Rais Kenyatta.
''Tunaweza
kufanya vizuri zaidi tukiwa katika kanda kuliko nchi mojamoja,'' aliongeza
Rais.
Naye
Katibu Mkuu wa EAC, Dk Sezibera alimpongza Rais kwa kushinda uchaguzi wa rais
hivi karibuni na kuwashukuru pia wananchi wa Kenya kwa kuwa mfano wa kuigwa kwa
jinsi walivyoendesha uchaguzi huo.
0 comments:
Post a Comment