"KARIBU BEIJING", Balozi wa Tanzania nchini
China, Philip Marmo (kulia) akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, China, baada ya Kinana
na ujumbe wake kuwasili akitokea jimbo la Sichuani, leo Machi 17, 2013. Kinana
na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini china kwa ziara ya siku kumi ya
mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China.
Balozi wa Tanzania Nchini China, Philip Marmo
akizungumza baada ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na
ujumbe wake, nyumbani kwake, kwenye Ubalozi wa Tanzania mjini Beijing, China,
baada ya kuwasili leo Machi 17, 2013, akitokea jimbo la Sichuan. Kinana
na ujumbe wa viongozi 14 wa CCM wapo nchini China kwa ziara ya siku kumi ya
mafunzo, kwa mwaliko wa Chama CHa Kikomunisti cha China. Kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Baadhi ya Watanzania waliopo jijini Beijing, China
wakichangamkia kupigapicha na Katibu wa NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dk. Asha-Rose Migiro (Katikati) nyumbani kwa Balozi wa Tanzania nchini China.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge
wa Busega, Dk. Titus Kamani akiwasalimia baadhi ya Watanzania wanaoishi Beijing
China, baada ya kuwasili na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, nyumbani wa
Balozi wa Tanzania nchini China, Philp Marmo, Machi 17, 2013. Kamani ni
miongoni mwa viongozi 14, wa CCM waliopo katika msafara wa Kinana ambaye yupo
nchini China na ujumbe huo kwa ziara ya Kikazi nchini humo, kufuatia mwaliko wa
Chama Cha Kikomunisti cha China.
Baadhi ya Watanzania wanaoishi Beijing, wakilaki
Kinana na msafara wake, nyumbani kwa Balozi Marmo, Beijing China, leo Machi 17,
2013. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Beijing,
Daninga .Daniel
0 comments:
Post a Comment