Na
Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Advanced security Limited imeingia makubaliano na bingwa wa
dunia wa mchezo wa Kareti, Profesa Maurizio Martina wa Italia kwa ajili
ya kutengeneza filamu mbalimbali pamoja na ile inayopinga mauaji ya walemavu wa
ngozi, albino na unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake.
Makubaliano
hayo yalifanyika jana kwenye hotel ya JB Delmonte na filamu hiyo itaanza
kurekodiwa ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa na kukamilika kwa miezi mitatu.
Mwenyekiti
wa Kampuni ya Advanced Security Limited, Juma Ndambile alisema kuwa
sababu kubwa ya kuingia katika masuala ya filamu ni moja ya shughuli zake
katika kujihusisha na masuala ya jamii.
Ndambile
alisema kuwa kampuni yao ni Limited na kutokana na hilo inaweza kufanya
shughuli nyingine mbalimbali tofauti na huduma ya ulinzi na usalama.
Alisema
kuwa katika filamu hiyo, atawashirikisha waigizaji mbali mbali wa hapa nyumbani
na wapo mbioni kukamilisha taratibu zote kwa mujibu wa sheria ya kurekodi
filamu hapa nchini.
Kwa
mujibu wa Ndambile, Profesa Maurizio ambaye ameigiza filamu nyingi
katika nchi za mbali mbali pamoja na Uingereza na Marekani mbali ya Italia
atashirikiana na mke wake, Angel Howel na mwanaye, Dumiano ambaye amewahi
kuigiza na mcheza filamu maarufu duniani.
Profesa
Maurizio alisema kuwa pia atafundisha wanawake jinsi ya kujilinda kwa kutumia
mchezo wa karate ili kuondoa unyanyasaji wa wanawake nchini.
Amesema kuwa
amefanya kazi hiyo nchi mbali mbali ikiwa pamoja na DR Congo na Afrika
Kusini.
“Lengo la
filamu yangu ni kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na mila potofu za kuwaangamiza
albino na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake,” alisema Profesa Maurizio
ambaye pia ni Rais wa Dunia wa Shirikisho la Mchezo wa Kareti.
Maelezo ya picha
Bingwa wa Dunia wa mchezo
wa Karate ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la mchezo huo duniani, Professa
Maurizio Martina akionyesha moja ya mbinu atakazozitumia kuwafundisha albino na
wanawake kwa lengo la kujilinda wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana
uliofanyika kwenye hotel ya JB Delmonte.
0 comments:
Post a Comment