1. Kamati ya Uchafguzi ya TFF imepitia mchekato
mzima we uchaguzi we Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Uchaguzi wa
Tanzania Premier League Board (TPL Board) ili kujiridhisha kuwa mchaketo mzima
wa uchaguzi unakidhi kikamilifu matakwa
ya Kanuni za Uchaguzì na Katiba ya TTF. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imebaini kuwa
kuna matatizo ya kikanuni ambayo yanapaswa kuzingatiwa kwemza kabla ya
kuendelea na mchakato wa uchaguzi.
2. Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 10(5) ya Kanuni za
Uchaguzi za TFF INASITISHA zoezi la uchaguzi wa Tanzania Premier League Board
(TPL Board) na Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hadi
hapo matatizo hayo ya kikanuni yatakapopata utatuzi.
3. Kamati ya Uchaguzi itawatangazia baadae
tarehe mpya za uchaguzi wa
Tanzania Premier League Board (TPL Board) na
Shirikisho la Mpira we Miguu Tanzania (TFF).
Deogratias Lyatto
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TFF
0 comments:
Post a Comment