Mwenyekiti
wa Kamati ya maandalizi ya Tuzo za Mwanamichezo bora wa TASWA, Haji
Manara, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, leo
mchana, wakati wakitangaza kuhusu kusogezwa mbele kwa shughuli hiyo ya
utaoji tuzo ambapo sasa hafla hiyo itafanyika April 27, 2013, ambapo pia
alizungumzia kwa ujumla maandalizi hayo. Katikati ni Katibu Mkuu wa
TASWA, Amir Mhando, (kulia) ni Mjumbe wa TASWA, Turo Chambo.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano huo, leo.
*******
TUZO
za Wanamichezo Bora wa Tanzania wa mwaka 2012 zinazoandaliwa na Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) zitafanyika Aprili
27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kamati
inayoratibu tuzo hiyo ilifanya kikao chake cha kwanza Jumanne wiki hii,
ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikubaliana mambo mbalimbali ya
kimsingi kuhakikisha tuzo zinakuwa na mvuto kama ilivyokuwa miaka
iliyopita na pengine ziwe bora zaidi.
Kutokana
na hali hiyo vyama vyote vya michezo vilivyosajiliwa na Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), ambavyo vipo hai na vinaendesha mashindano
vitaandikiwa barua kwa ajili ya kutoa mependekezo yao ya wanamichezo
waliofanya vizuri kwa mwaka jana upande wa michezo yao na yawasilishwe
kabla ya Februari 28, mwaka huu.
Tunaomba
ieleweke kuwa vyama vitatoa mapendekezo na hivi sasa Kamati ya Tuzo
inafanya mazungumzo na kampuni mbalimbali zinazohusika na mambo ya
mawasiliano ili kuona namna zitakavyoshirikiana na wadau katika
kuchambua majina hayo, ambapo kila chama kimetakiwa kiwasilishe majina
matano ya wanamichezo wao kwa kila jinsia kama ni mchezo unaochezwa na
jinsia mbili, lakini kama ni mchezo wa jinsia moja watatakiwa
kuwasilisha majina matano ya jinsia husika tu.
Yapo
marekebisho kadhaa yamefanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya
tuzo kutoka 36 za mwaka jana hadi kufikia 42 mwaka huu na idadi inaweza
kuongezeka ama kupungua kulingana na sifa za wanamichezo ambazo vyama
vitaleta.
Tunaomba
wadau watupe ushirikiano wa kutosha katika jambo hili ili kuzifanya
tuzo ziwe bora na kuhakikisha kila anayestahili kupata tuzo anazawadiwa
kwa kuthamini kile alichokifanya, ambapo ukumbi utakapofanyika tuzo hizo
utatangazwa hivi karibuni baada ya kukamilisha baadhi ya mambo.
Idadi
ya michezo itakayopewa tuzo pamoja na aina nyingine ya tuzo
zitakazotolewa ikiwemo Tuzo ya Heshima tutaendelea kujulishana kadri
siku zitakavyokuwa zinasonga mbele. Washindi wa kila tuzo ndiyo
mmojawapo ataibuka kuwa Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2012.
Dhamira
ya kamati yangu ni kutaka kuhakikisha kuwa TASWA haikukosea kututeua na
tutaleta wanammichezo sahihi na hatimaye kumpata yule bora ambaye
ataungana na wengine waliopata kutwaa tuzo hiyo miaka ya nyuma.
Wanamichezo ambao wamepata kutwaa Tuzo ya Mwanamichezo Bora Mwaka wa Tanzania ni Samson Ramadhan (2006), Martin
Sulle (2007) na Mary Naali (2008) wote wakiwa wanariadha, wakati mwaka
2009 alikuwa Mwanaidi Hassan na mwaka 2010 alikuwa pia Mwanaidi Hassan
ambaye ni mcheza netiboli na mwaka 2011 alikuwa mwanasoka Shomari
Kapombe.
Haji Manara
Mwenyekiti Kamati ya Tuzo za TASWA
01/02/2013
0 comments:
Post a Comment