Mwakilishi
wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA) Bishara Al
Masroori akizungumza na Wazazi wa watoto wenye ulemavu hawapo pichani
katika hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao,kushoto ni Waziri wa Nchi
Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji huko Makao
Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Weles.
Waziri
wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Fereji akiwa na
Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada Bishara Al
Masroori wakimkadhi baskeli ya walemavu Mtumwa Hamadi Khamis mkaazi wa
Tomondo huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu
Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
*******
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar 1/2/2013
Waziri
wa Nchi Afisi ya Makamu wa kwaza wa Rais Fatuma Abdullhabibu Fereji
amesema kuna kila sababu za kuwasaidia Vipando watu wenye ulemavu ili
waweze kufikia katika Shughuli zao na kuungana na wenzao katika harakati
za maisha.
Hayo
ameyasema leo huko Makao makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu
Zanzibar Welesi alipokuwa akikabidhi Baskeli za kutembelea na vifaa
mbali mbali kwa Watoto wenye ulemavu, ukiwa ni msada kutoka Jumuiya ya
Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA).
Amesema
msaada wa Jumuiya ya ZANCANA unafaa kuigwa na kupigiwa mfano kwani
utawawezesha Walemavu hao kukabiliana na majukumu yao ya kila siku kwa
wepesi.
Waziri
Fereji amesema Walemavu wanahitaji kufanya mambo mengi ya msingi lakini
kuna wakati hushindwa kutokana na ukosefu wa usafiri ikiwa ni pamoja na
Baskeli na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia kufanya mambo yao
ipasavyo.
“wana
hitaji kwenda skuli,kutembea, kuchanganyika na wenzao,hivyo wanapo kosa
vifaa kama hivi husindwa watoto wetu kuyafikia mahitaji yao muhimu
hivyo msada huu ni furaha kwao na kwetu” Alisema Waziri Fereji.
Aidha
waziri huyo asema kuwa watu wenye ulemavu wanahitaji kutunzwa na kupewa
haki za msingi ikiwemo elimu,afya, malazi, chakula na mengineo kitu
ambacho mtu yoyote anaweza kuwawezesha watu hao si lazima wazee .
Amesema
mpaka hivi leo kuna badhi ya Wazazi wanawafungia ndani walemavu na
kuwakosesha haki zao za msingi kwa madai kuwa ni hawataweza kufikia
masafa ambayo huduma zinatolewa.
Waziri
Fereji amekemea tabia hiyo ya kuwafungia Walemavu na kusisitiza kuwa
ulemavu si sababu ya kumkosesha mtoto elimu kwani jambo hilo liko katika
milki ya Mwenyezi mungu Muumba.
Nae
Mzazi wa mtoto Mtumwa Hamad Khamis wakati akitoa shukrani alisema
Msaada huo umekuja wakati muafaka kwao kutokana na kukosa Baskeli ambazo
watoto wao walikuwa wanazihitaji kwa muda mrefu.
Ameongezea
kuwa mtoto wake amekuwa akipata wakati mgumu wakati wa kwenda Skuli
kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao unamuwezesha kwenda na
kurudi Skuli anayosoma.
Aidha
mzazi huyo amegusia suala la unyanyapaa linalomkabili Mtoto wake
Skulini kwao kutokana na Skuli hiyo kutokuwa ya mchanganyiko kati ya
Wanafunzi Walemavu na wasiokuwa Walemavu jambo ambalo linamfanya
afikirie kubadilisha Skuli.
Jumuiya
ya Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA) imetoa msaada kwa Watu
wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na Bskeli za kutembelea, Viti, vifaa
watoto vya kuchezea ikiwa ni jitihada za kusaidia ndugu zao wanaoishi
katika mazingira magumu .
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.
0 comments:
Post a Comment