Mkurugenzi
wa kinywaji cha Nzagabwa Kiroi Suma (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza Eng.Evarist Ndfikilo alipo tembelea kiwanda hicho katikati ni Mkuu wa
kiwanda cha Nzagamba Bw.Patrick Phiri.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Eng.Evalist Ndikiro akitembelea kiwanda cha kinywaji aina ya
Nzagamba wa pili Kushoto ni Kilowi Suma Mkurugenzi wa tatu ni Nyamoronga John
Meneja uzalishaji wa nne ni Ashraf Gugu meneja mauzo .
***** *******
Na Mwandishi Wetu
KIWANDA kipya cha kuzalisha bia ya asili
ijulikanayo Nzagamba kimefunguliwa rasmi jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Mhandisi Evaristi Ndikilo.
Kiwanda hicho ambacho kipo chini ya Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL), kitajihusisha na kutengeneza bia hiyo ya asili, ambayo
tayari imeanza kupokelewa kwa shangwe na wenyeji wa Kanda ya Ziwa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho,
Mhandisi Ndikilo alisema, amefarijika mno kuona kimejengwa Mwanza, kwani
kitachangia kwa kiasi kikubwa mapato ya mkoa huo.
“Niwapongeze sana wenzetu wa Nzagamba kwa kuja
na wazo zuri kama hili la kuanzisha bia ya asili, tena wakaipa jina lenye asili
ya Kanda ya Ziwa hususani kabila la Wasukuma.
“Hii imenifurahisha. Lakini kikubwa zaidi ni
uamuzi wa kukiweka kiwanda hiki hapa Mwanza, kwa sababu mlikuwa na uwezo
wakuamua kujenga mkoa mwingine wowote ule lakini mkatoa upendeleo wa dhati kwa
mkoa wetu. Kwa uamuzi huo tunashukuru sana,” alisema.
Aliwataka wananchi kuhakikisha wanaonyesha
uzalendo wa dhati kwa kupenda kutumia vitu vya asili, huku akitolea mifano ya
nchi za Zambia na Malawi, ambapo bia za asili zinapewa nafasi kubwa.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Nzagamba, Kirowi Suma
naye alisema watahakikisha wanazalisha bidhaa bora zaidi na kuwataka Watanzania
wapende vitu vya asili ili kuonyesha uzalendo wao.
“Kwetu Nzagamba tunaamini tutaendelea kupigania
ubora wa bidhaa yetu na naomba Watanzania watuunge mkono kwa kuipa nafasi bia
hii ya asili,” alisema Suma.
Nzagamba tayari imeanza kusambazwa, huku
ikipokelewa vizuri zaidi na watumiaji, kutokana na kuwekwa katika ubora
unaotakiwa.
0 comments:
Post a Comment