Wakiwa katika picha ya pamoja watoto ambao ni mapacha watatu, Rehema, Amani na Neema.
Na Kalisa Kachuchu wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Edwin Rweyongeza, amewaomba Watanzania kumsaidia kuwatunza watoto wake mapacha watatu ili waweze kukua vizuri kutokana na matatizo ya kipato yanayomkabili.
Rweyongeza, aliitaja misaada hiyo kuwa ni pamoja na Chakula cha watoto lishe, yakiwamo maziwa pamoja na matibabu ya kuishiwa na damu yanayoendelea kuwa tatizo kwa watoto wake.
Akizungumza muda mfupi uliopita na Habari na Matukio Blog, Rweyongeza alisema ukosefu wa kipato unaomsumbua, unamfanya ashindwe kuwamudu watoto hao waliozaliwa Julai sita mwaka 2011 katika Hospitali ya Mwananyamala.
Alisema kutokana na ukosefu wake wa kipato, Ustawi wa Jamii wilaya ya Kinondoni, ilikubali Rweyongeza apate msaada kutoka kwa jamii, kwa barua yao waliyoandikaa Septemba 14, mwaka 2011 yenye kumbukumbu namba W/WG/2011 na kusainiwa na A.Mbusa.
“Naomba msaada kutoka kwa Watanzania wenzangu na Dunia kwa ujumla ili watoto wangu waweze kupata lishe na kufanikisha maisha yao, maana mimi baba yao kwa sasa sina kipato chochote kwasababu sina kazi ya kuniingizia kipato.
“Kama ningekuwa na uwezo nisingeomba msaada, ukizingatia kwamba watoto watatu kuwalea ni kazi kubwa, hasa kwa masuala ya lishe na matibabu, kama vile maziwa na mengineyo yanayochangia kukua vizuri,” alisema Rweyongeza.
Kwa wenye moyo nahitaji la kumsadia, kijana huyo mwenye miaka 29, alizitaja namba zake ni 0767 646599, 0719 909085, huku akitanguliza shukrani zake za dhati kwa Watanzania wote.
Mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Edwin Rweyongeza akiwa na familia yake kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment