Mkurugenzi
wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Paulina
Mkonongo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David
Mgwasa wakisalimiana na wanafunzi wanaosomeshwa na Kampunihiyo chini ya Mpango wa
kumuelimisha Mtoto wa Mkulima wa Zababu unaojulikana kama ‘Zabibu na Shule
kwanza’. Jumla ya wanafunzi 30 wanasomeshwa na Kiwanda cha Konyagi na
wametembelea jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kimafunzo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya
Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David Mgwasa akizungumza jambo na pamoja
nae ni baadhi ya viongozi wa Kampuni hiyo .
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni
watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David Mgwasa akizungumza jambo wakati wa mkutano na Viongozi wa Wizara ya Elimu.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni
watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David Mgwasa akizungumza katika mkutano na wanahabari katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara ya Elimu jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Paulina Mkonongo.
Mmoja wa wanafunzi hao akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Elimu ya Sekomdari na Uongozi wa Konyagi.
Mpango
huu wa kusomesha watoto wa mkulima unaojulikana kama “Zabibu na shule kwanza” ulizinduliwa rasmi mnamo tarehe 01 Julai
2011 Bungeni Dodoma na Spika wa bunge la Tanzania, mama Anna
Makinda.
Lengo
kuu la mradi huu ni kuhakikisha familia za wakulima walio kwenye mkataba na TDL
wanafaidia na kazi za wazazi wao kwa kusaidia watoto wa familia hizo kwenda
shule, kupunguza idadi kubwa ya watoto wanaoshindwa kuendelea na elimu ya
sekondari kutokana na kukosa pesa za kulipia ada na mahitaji muhimu ya
shule kutoka kwa wazazi ama walezi wao ambao ni wakulima wa zao la zabibu.
TDL
itakuwa imewapunguzia mzigo mkubwa na kuwapa wakulima hawa muda muafaka wa
kujitatiti zaidi katika shughuli za kilimo cha zabibu ili kuziwezesha
familia zao kujikimu vizuri kimaisha.
Mradi
huu ulianza na watoto kumi (10), na mwaka jana tukaongeza watoto ishirini (20) na
ni matarajio kuwa mwaka huu idadi ya watoto watakaopewa ufadhili itakuwa
wanafunzi ishirini (20), hivyo kufikisha idadi ya wanafunzi wanaosomeshwa na
mpango huu kuwa wanafunzi hamsini (50).
TDL
kama kampuni tunaamini kuwa, uwekezaji kwenye elimu na pia kumsomesha
mtoto ni kukuza uchumi wa nchi yetu.
0 comments:
Post a Comment