Serikali ya Jamuhuri ya
muungano wa Tanzania, kupitia Baraza la Sanaa la Taifa, limebariki kufanyika
kwa Fainali za Taifa za Miss Utalii Tanzania 2012/13 baada ya kuridhishwa na
maandalizi yaliyo fanywa na Miss Tourism Tanzania Organisation waandaaji wenye
dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano hayo kitaifa na kimataifa,
pia kwa kuzingatia sheria za nchi, kanuni na Taratibu za mashindano.
Serikali pia imeridhishwa
na jinsi Fainali za ngazi za mikoa na kanda zilivyofanyika kwa afanikio,ambapo
kila mkoa umepata washindi wenye sifa za kuwakilisha mkoa husika katika Fainali
za Taifa mwaka huu,ambapo jumla ya warembo 60 waingia rasmi kambini kesho
katika hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, kuanza mbio za kuwania Taji hilo
la Taifa.
Washindi wa 1-5 wa Fainali
za Taifa ,watawakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Dunia yakiwemo
ya International Miss Tourism World, Miss Tourism United Nation, Miss Heritage World,
Miss Tourism University World, Miss Globe International.
Miss Utalii Tanzania ,hadi
sasa tunashikilia Jumla ya mataji 5 ya Dunia na kimataifa, yakiwemo ya Miss
Tourism World 2005-Africa,Miss Tourism World 2006-SADC,Miss Tourism World
2007-Africa, Miss Tourism Model Of The World 2008-Personality.
Fainali za Taifa mwaka huu
zimepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Februari ,wilaya ya Temeke na mkoa wa
Dar es Salaam ukiwa umepewa heshima ya kuwa wenyeji wa Fainali hizo.
0 comments:
Post a Comment