Mwaka ulioisha hivi karibuni umeonyasha, baada ya miaka
mingi, kuongezeka kwa chuki katika jamii ambayo awali ilikuwa inaishi kwa amani
kati ya Waislamu na Wakristu Afrika Mashariki. Mwandishi Isaac Mwangi wa Shirika Huru la
Habari la Afrika Mashariki (EANA) anatathmini hali hiyo isiyo ya kufurahisha ya
mgogoro kati ya Waislamu na Wakristu ambayo ilitia doa la
mahusiano mwaka jana…Hii hapa taarifa yake.
Arusha Januari 15, 2013 (EANA) -
Agosti 27, Kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu nchini
Kenya, Shehe Aboud Rogo aliuawa kwa kupigwa risasi ndani ya gari lake mjini
Mombasa.Vijana wa Kiislamu katika mji huo wa ukanda wa Pwani walianzisha ghasia
mara moja baada ya tukio hilo ambapo waliharibu na kuchoma moto makanisa katika
vurugu za kiimani mbaya zaidi kuwahi kutokea katika nchi Kenya. Viongozi wa dini
toka pande zote mbili walijaribu kwa kila hali kuwasihi wafuasi wao na kurejesha
tena utulivu katika eno hilo.
Lakini tukio hili ni la pekee zaidi ambapo lilishuhudia
uvumilivu wa dini tofauti ukiwa umejaribiwa kwa kiwango cha juu kwa mwaka 2012
kwa nchi za Kenya na Tanzania.
Mapema,Jumapili ya Julai mosi,mabomu mawili yalirushwa
kwa waumini waliokuwa wanasali katika makanisa mawili tofauti, enee la
Garisa,katika mkoa wa Kaskazini Mashariki unaopakana na nchi ya Somalia. Jumla
ya watu 17 walikufa, wakiwemo polisi wawili waliokuwa wanalinda moja ya makanisa
hayo.Pia waumini 60 walijeruhiwa.
Kiongozi huyo wa Kiislamu, Shehe Rogo aliyeuawa, awali
alitamka wakati wa swala ya Ijumaa msikitini mjini Mombasa kufuatia mashambulizi
hayo ya Garisa kwamba tukio hilo lilifanywa na Waislamu kulipiza kisasi. Polisi
hawakumkamata.
Wakati tukio hilo lilitoa ishara ya Waislamu kuishi kwa
mashaka na Wakristu nchini Kenya, hali kama hiyo ya mashambulizi ya moja kwa
moja haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka lukuki.
Wiki tatu baada ya mashambulio ya Garisa,polisi nao
walikamata mabomu yaliyokuwa yanadaiwa kuwa yangetumika kulipua kanisa Katoliki
la Assumption of Mary, katika Parokia ya Umoja, jijini Nairobi. Watu wawili
waliokamatwa na mabomu hayo waliripotiwa kuwa waliyaingiza mabomu hayo kutoka
nchi moja jirani na Kenya.
Kwa upande mwingine wa mgawanyiko huo kwa misingi ya
kidini, kulikuwepo pia kupamba kwa uhasama miongoni mwa jamii za Waislamu
wenyewe.Jarida la kila wiki linalochapishwa na Jamia Mosque mjini Nairobi la The
Friday Bulletin,liliripoti Agosti kwamba waislamu wenye imani kali walibomoa
msikiti mmoja katika wilaya Kajiado,kumwagia kinyesi msikini na kuchoma moto
nakala za Korani, Kitabu Kitakatifu cha Waislamu. Msikiti huo ulikuwa unajengwa
eneo la Olkejuado High School, ulikuwa unakaribia kukamilika.
Katika tukio la pili,Mwalimu Mkuu wa Kangeta High
School, Meru aliwatimua wanafunzi 15 baada ya kusisitiza kufunga wakati wa mwezi
wa Ramadhani, hivyo kwenda kinyume na amri ya mkuu wao wa shule.
Kujihusisha kwa Kenya, kijeshi nchini Somalia tangu
Oktoba 2011, ambako jeshi la nchi hiyo linapambana na kundi la wanamgambo la Al
Shabaab lilifungulia kuliongeza kwa matukio ya kigaidi.Mashambulio hayo kwa
kiasi kikubwa yalifanya hali ya uhasama kuwa mbaya zaidi 2012 kati ya dini hizo
mbili kuu nchini Kenya za Kikristu na Kiislamu.
Nchini Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda alitiwa mbaroni
Oktoba baada ya waandamanaji wa Kiislamu kutaharuki na kuchoma makanisa matano
jijini Dare es Salaam.
Ghasia hizo zilizuka baada ya mvulana wa Kikristu
kudaiwa kukojolea nakala ya Korani. Zaidi ya watu 120 walitiwa mbaroni kufuatia
ghasia hizo, ambazo zilijenga uhasama mkubwa kati ya Waislamu na Wakristu,
katika moja ya matukio mabaya zaidi ya kidini kuwahi kutokea katika historia ya
Tanzania bara.
Kulikuwapo pia ghasia katika kisiwa cha Zanzibar wakati
kiongozi mmoja wa dini ya Kiislamu, Shehe Farid Hadi Ahmed alipotekwa asubuhi ya
Oktoba 16. Kanisa la Jimbo la Christ Church lilipo eneo la Mji Mkongwe kisiwani
hapo lilishambuliwa na waamini wake kuondolewa haraka ili
kuwanusuru.
Uganda haikupata matukio ya migogoro
mikubwa ya kidini kama ilivyokuwa kwa Kenya na Tanzania.Lakini Mwinjilisi wa
kanisa la Pentekoste, ambaye aliwashawishi maelfu ya waumini ya Kiislamu
kujiunga na Ukristu aliharibiwa uso wake wakati wa usiku wa Krismasi 2012, tukio
ambalo lilileta hofu baina ya waumini wa dini hizo mbili pia.
Kwa nchi za Rwanda na Burundi hapakuripotiwa matukio
yoyote yasiyo ya kawaida yaliyoleta mvurugano baina ya Waislamu na
Wakristu.
0 comments:
Post a Comment