Mtoto Simoni Mlope
Kulia ni mama wa mtoto Simoni Mlope ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa
tundu kwenye moyo na kulazimika kukatisha masomo yake ya shule ya
msingi. Hapo yupo nyambani kwake maeneo ya mahenge alipotembelewa na
waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma.
Mtoto Simon Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la mahenge katika manispaa ya
songea mkoani Ruvuma amelazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa
darasa kwanza kutokana na mototo huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo .
Mtoto
simon Mlope alikubwa na ugonjwa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya
kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo
inasababisha kuvuta pumzi kwa shida.
Mama
wa mototo simon mlope anayeitwa AMINA ALLY anawaomba watanzania
kumsaidia mtoto wake fedha za matibabu Baada ya kuambiwa na madaktari
kuwa simon anatakiwa kwenda nchini india kutibiwa,baada ya kupata rufaa
kutoka muhimbili mwaka 2006 huku familia yake ikiwa haina uwezo kabisa.
Majirani
wa familia ya simon nao wanasema kuwa mototo simon anahitaji msaada wa haraka
kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania wamsaidie.
Kinachosikitisha
zaidi baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la SIMON MLOPE
ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni
alisema yuko nchini Msumbiji.
Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia SIMONI MLOPE atumie simu namba 0752732290.SOURCE: DAMASHO NEWS
0 comments:
Post a Comment