Mkurugenzi
wa Mad Mad Entertainment, Yasmin Razak (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kampuni yake kuingia
mikataba na wasanii wa filamu wa Tanzania watakaokwenda Nigeria na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya kutengeneza filamu.
Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga
na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
Msanii wa filamu, Steve Nyerere (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.Kushoto
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Superior, Issack Kasanga na Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba.
*****
KAMPUNI ya Mad Mad
Entertainment iliyopo jijini London nchini Uingereza, imeanzisha program
maalum ya kupeleka wasanii wa filamu za bongo nje ya nchi kwa lengo la
kukuza sanaa hiyo hapa nchini.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo Yasmin Razak alisema ameamua kufanya kazi na wasanii hao
ili kuleta mabadiliko na kuwakwamua kiuchumi wasanii wa filamu hapa
nchini.
“Kwa muda mrefu
niliokaa London sioni kama sanaa hii ina maendeleo, nikafikiria kitu gani
nifanye ili kukuza tasnia hii, katika mkataba na kampuni msanii atakayetengeneza filamu na wasanii wa
nje atalipwa kiasi cha sh 50 milioni pamoja na malipo mengine
yatakayokuwepo kwenye mkataba, ikiwa ni pamoja na asilimia fulani kwa kila
kazi itakayouzwa hapa nchini.
“Nimekuwa nikifanya kazi hiyo na
wasanii wengi kutoka Nigeria wakiwemo kina Omotola, Two Face na wengineo
na pia Ghana, Congo na hata Uingereza, hivyo nimeonelea kuwa itakuwa vema
Tanzania nao kuingia katika mchakato huo,”alisema Razak.
Razak ambaye amewahi kufanya kazi ya filamu na Fally Ipupa, alitaja vigezo vya msanii atakayechaguliwa ikiwa ni pamoja na umaarufu, kuijua lugha ya kiingereza, uwezo wa kuigiza na kuuvaa uhusika wowote pamoja na mavazi.
Naye rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba aliwataka wasanii hao kujipanga katika kuhakikisha wanaingia kwenye ushindani huo na kuwataka wale watakaochaguliwa kujituma na kuonyesha nidhamu ya uhakika.
“Hapa kuna kuinua vipaji, soko la
kimataifa na mengineyo, hivyo ni vema kufanya kazi kikamilifu kwa wale
watakaochaguliwa na si kujisahau, wanatakiwa wasanii watatu na tupo katika
hatua za awali za mchujo,” alisema
Mwakifamba.
Naye muigizaji Issa Musa maarufu kama Cloud, alisema kuwa lugha itakuwa ni tatizo kubwa kwa wasanii walio wengi, hivyo kuitaka kampuni hiyo iangalienamna ya kuweza kuwasaidia wasanii hao.
0 comments:
Post a Comment