Mahmoud Ahmad Arusha
TAASISI ya utafiti wa wanyama Pori nchini yenye makao makuu yake mkoani Arusha (TAWIRI),imepokea majokofu mawili makubwa yatakayosaidia kupunguza changamoto waliokuwa nayo ya upungufu wa majokofu ya kuhifadhia sampuli mbalimbali zinazotokana na tafiti mbalimbali za wanyama pori.
TAASISI ya utafiti wa wanyama Pori nchini yenye makao makuu yake mkoani Arusha (TAWIRI),imepokea majokofu mawili makubwa yatakayosaidia kupunguza changamoto waliokuwa nayo ya upungufu wa majokofu ya kuhifadhia sampuli mbalimbali zinazotokana na tafiti mbalimbali za wanyama pori.
Kaimu mkurugenzi wa utafiti,Dkt Julias Keyu alisema kuwa msaada huo ambao ni pamoja na kompyuta mbili aina ya Laptop, umetolewa na kampuni ya Samsung Elektronics tawi la Afrika mashariki,chini ya ushirikiano wa Kituo cha utafiti wa mali asili cha nchini Korea.
Alisema kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka kwani kabla ya hapo taasisi hiyo ilikuwa ikikabiliwa tatizo kubwa la upungufu wa majokofu kutokana na yale yaliyokuwapo kujaa sampuli katika maabara zake hasa maabara kuu iliyopo Serengeti mkoani Mara yenye majokofu mawili tu.
Dkt Keyu aliongeza kuwa taasisi hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa vitendea kazi pamoja ukubwa wa gharama za uwendeshaji tafiti ,huku akitolea mfano kwamba mnyama mmoja anaweza kugharibu hadi dola 100 kumfanyia utafiti.
Alisema ili kukabili changamoto hiyo taasisi hiyo inahitaji majokofu makubwa 10 ,tofauti na yaliyopo sasa ambayo ni matano ,katika kuhifadhi sampuli mbalimbali za wanyama kwani sampuni hizo huchukua muda mrefu kuhidhadhiwa wakati wa utafiti.
Alisema lengo la kufanya utafiti wa wanyama ni kutambua vizazi vya wananyama,mlipuko wa magonjwa kutoka kwa mnyama kwenye kwa binadamu na kutambua vimelea vya magonjwa ya wanyama Pori pamoja na uhifadhi endelevu wa uoto wa asili na wanyama pori.
Dkt.Keyu aliyetaka makampuni hapa nchini na nje ya nchi kuona umuhimu wa kusaidia taasisi hiyo katika kuipatia vifaa vya utafiti ili ili kufikia malengo ya tafiti za aina mbalimbali,katika hatua nyingine dkt Keyu kuwasihi binadamu kuacha mwingiliano na wanayama ili kuepuka kuambukizwa na magonjwa mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment