Na James Gashegu, EANA
Mwaka uliomalizika wa 2012 imeshuhudia ucheleweshwaji
wa aina yake katika mipango ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
ikiwa ni pamoja na kusogezwa mbele kuanzishwa kwa Umoja wa Fedha ambao sasa
unatarajiwa Novemba mwaka huu.
Yafuatayo
ni matukio mengine muhimu kwa EAC kwa mwaka uliopita kama yalivyofuatiliwa na
Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki(EANA)
EAC yapata ofisi zake za kudumu
Mwaka
2012 utaendelea kukumbukwa katika historia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
kuwa ni mwaka ambao taasisi hiyo ya kanda ilihamia katika ofisi zake za kudumu
baada ya miaka mingi ya kukodi ofisi ghali za Kituo cha Mikutano ya Kimataifa
cha Arusha (AICC).
Makao
makuu ya EAC yana ofisi zake sasa zenye eneo la mita za mraba 15,025 na majengo
matatu yenye ghorofa nne kila moja.
Ujenzi
wa ofisi hizo ulizinduliwa na wakuu wa nchi tano zinazounda jumuiya hiyo ikiwa
ni pamoja na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi Novemba 20, 2009,
ingawaje ujenzi rasmi ulianza Januari 28, 2010.
Mradi
huo umefadhili wote kwa ujumla wake na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa
gharama ya Euro 14.8 milioni.
Margret Zziwa Nantongo achaguliwa Spika wa bunge la
EAC
Margret
Zziwa Nantongo alichaguliwa na wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kuwa
Spika wa Bunge hilo baada ya kumshinda mganda mwenzake,Dora Byamukama.
Spika
huyo mpya ambaye aliapishwa na Katibu wa Bunge hilo, Kenneth Madete mara baada
ya uchaguzi huo alinyakua ushindi wa kura 33 katka raundi ya pili ya upigaji
kura.
Byamukama
kwa upande wake aliambulia kura 12 ikiwa ni chini kutoka kura 18 alizopata
katika raundi ya kwanza.
Mbuge
huyo wa EALA amechukua nafasi ya uspika iliyoachwa wazi na Mkenya, Abdulaihin
Abdi aliyeshikilia nafasi hiyo kwa miaka mitano, akirithi kutoka kwa mtanzania,
Abdurahman Kinana.
Katika
kikao cha kwanza cha Bunge la tatu kilichokaa Nairobi,Kenya Zziwa alikiri
kwamba licha ya utekelezaji wa mihimili ya awali ya mtangamano- Umoja wa
Forodha na Soko la Pamoja, changamoto nyingi za utekelezaji wa mtangamano mzima
bado zinaendelea kuwapo. Miongoni mwa changamoto alizozitaja ni pamoja na
vikwazo vinavyokwamisha utendaji wa biashara ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa
vizuizi visivyo na kodi na ugoigoi wa agenda mpya katika sera za kitaifa kuhusu
EAC.
Mabunge ya kitaifa yakubali kuanzisha kamati za
kushughulikia masuala ya mtangamano
Katika
mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Afrika Mashariki mjini Kigali, Rwanda Mei
2012,mabunge yote ya kitaifa katika kanda hiyo yamekubaliana kuanzisha kamati
maalum kushughulikia masuala yanayohusu mtangamano wa kikanda na kutenga muda
maalum ili kujadili masuala hayo kama ilivyo katika kamati zilizopo katika
mabunge ya kitaifa.
Barabara ya Arusha-Namanga-Athi River iliyokarabatiwa
yazinduliwa rasmi
Wakuu
wa nchi za EAC Novemba 2012 walizindua rasmi barabara ya Arusha-Namanga-Athi
River iliyofanyiwa ukarabati mkubwa. Uzinduzi huo ulifanyika Athi River, nchini
Kenya.
Maombi ya Sudani Kusini, Somalia kujiunga EAC
yasogezwa mbele
Matarajio
ya Sudani Kusini na Somalia kujiunga na EAC yamesogezwa mbele baada ya wakuu wa
nchi za EAC kwa mara ya pili kuongeza muda wa kufanya maamuzi juu ya maombi ya
nchi hizo mbili kujiunga na jumuiya hiyo.
Katika
mkutano wao mjini Nairobi, wakuu wa nchi za EAC waliuagiza Mkutano wa Baraza la
Mawaziri kufanya majadiliano zaidi na nchi huru mpya ya Sudani Kusini ambapo
pia kuzingatia katika mammbo yaliyopatikana katika ripoti ya kamati kuhusu
Somali.
Hii
ni mara ya pili kwa maombi ya nchi hizo mbili kusogezwa mbele, la kwanza likiwa
la Aprili 2012 katika mkutano wa wakuu wa nchi wanachama mjini Bujubura,
Burundi.
Katika
mkutano wa mjini Nairobi pia wa wakuu wa nchi wanachama, Marais walipitisha
itifaki mbalimbali ikiwa ni pamoja na ya Amani na Usalama na ile ya Habari,
mawasiliano na mtandao wa teknolojia.
Kurahisisha usafirishaji bidhaa
Kwa
kipindi cha mwaka jana, kanda hii pia ilishuhudia kuanzishwa kwa Mradi wa
Uangalizi wa Usafirishaji ili kusimamia malori makubwa yanayosafirisha bidhaa
ndani ya kanda kwa kutumia vifaa vya kielektroniki kubaini sababu za
ucheleweshwaji katika njia zinazopitia.
Mpango
huo uliozinduliwa mjini Mombasa, Kenya unafadhiliwa na kampuni ya TradeMark
East Afica (TMEA) na kuasisiwa na Transit Transport Coordination Authority of
the Northern Corridor (TTCA) na Chama cha Wasafirishaji cha Kenya.
Katika
mradi huo, malori makubwa huwekwa vifaa vya kutambua mahali lilipo katika
safari yake (GPS) na ambacho kinarekodi kila mahali linaposimama katika safari
yake.Pamoja na kupewa kifaa hicho,madereva pia hupewa fomu za kujaza kwa nini
wamesimamishwa wakiwa safarini.
Mwaka
uliopita EAC imeshuhudia pia Rwanda kupitia Wazara yake inayoshughulikia
masuala ya mtangamano ikizindua sera yake ya kitaifa juu ya mwendendo wa
mtangamano wa EAC ili kufuatilia maslahi yake katika jumuiya hiyo.
Sera
hiyo mpya inalenga katika maeneo matano muhimu ikiwa ni pamoja na kuingiza
mtangamano wa kikanda katika maendeleo ya Rwanda, kuhusisha taasisi za
EAC,kupunguza na kulinda hatua zitakazolenga kupunguza athiri hasi kwa Rwanda
katika mwenendo mzima wa mtangamano.
Sera
hiyo pia inaangalia maeneo mengine ya kufanya maamuzi katika EAC na majukumu
yake na mfumo wa kitaasisi utakaoratibu, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa
mipango ya EAC nchini Rwanda.
Rwanda
inakua nchi ya kwanza katika jumuiya hiyo kuweka mkakati wa aina hii miongoni
mwa nchi tano za EAC.
Waziri
wa Masuala ya EAC wa Rwanda, Munique Mukaruliza alieleza kwamba kanda hiyo
inaendelea kukabiliana na changamoto za utekelezaji,hivyo kulazimika kuanzisha
juhudi kama hizo ili kuikabili hali hiyo.
Jessica Eriyo awa Naibu Katibu Mkuu mpya wa EAC
Naibu
Katibu Mkuu huyo, anamrithi Beatrice Kiraso, aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo
akishughulikia Shirikisho la Kisiasa na ambaye mhula wake wa pili wa kazi
ulikuwa umemalizika Uteuzi wa Eriyo ulithibitishwa katika kikao maalum cha 10
cha wakuu wa nchi za EAC kilichofanyika Arusha,Tanzania Aprili 28, 2012.
Katika
kikao hicho pia, mkataba wa kazi wa Naibu Katibu Mkuu, Jean Claude Nsengiyumva
aliyekuwa anashguhuikia Tija na Sekta ya Kijamii uliongezwa.
Mabalozi
vijana wa EAC
Ni
mwaka huo wa 2012 ambapo EAC kwa kupitia uungwaji mkono na Kituo cha EAC cha
Utafiti wa Amani cha Nyerere(NCPR) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Ujerumani (GIZ) walijitokeza na wazo la kuanzisha Mabalozi wa vijana wa EAC.
Mabalozi
Watano wa Vijana wa EAC (kutoka kila nchi mwanachama) waliteuliwa baada ya
kuibuka washindi bora kabisa katika mashindano ya kwanza wa Mdahalo wa
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu EAC juu ya Mtangamano wa Kanda.
Museveni achukua nafasi ya Uenyekiti wa EAC
Rais
Yoweri Museveni wa Uganda Desemba alichukua nafasi ya kuwa mwenyekiti wa
taasisi hiyo ya kanda ya EAC katika kipindi cha mwaka mmoja ujao katika kikao
cha kawaida cha 14 cha wakuu wa nchi wananachama EAC kilichofanyika mjini
Nairobi, Kenya.
Mkutano
huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Kenyatta pia
ulishuhudia kutiwa saini kwa barua yenye lengo la kukuza biashara baina ya EAC
na Marekani.
Rais
Museveni alimpongeza Rais Mwai Kibaki wa Kenya kwa kuliongoza jahazi la EAC kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa
upande wake, Rais Kibaki alisema miongoni mwa mafanikio ya EAC ni pamoja na
uanzishwaji wa Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja.
0 comments:
Post a Comment