WAWAKILISHI wawili wa klabu ya Seattle Sounders ya Marekani wataendesha semina kwa wadau wa michezo hapa nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.
Wawakilishi hao ni beki wa timu hiyo, Marc Burch (pichani juu) na kipa aliyestaafu ambaye kwa sasa ni mtangazaji , Kasey Keller .
Wakiwa
nchini, wachezaji hao wataendesha semina kwa vilabu vya Ligi Kuu ya
Tanzania Bara na shule za msingi katika siku na muda ambao utangazwa hapo baadaye. Z
iara hiyo ni moja ya kukuza ushirikiano baina ya Seattle Sounders na wadau
wa michezo nchini na ikumbukwe kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua
mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho Ngassa kucheza mechi ya kihistoria
dhidi ya timu ya Manchester United.
Kwa kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA), wawakilsihi wa timu hiyo pia watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani Arusha ikiwa pamoja na World Vision, taasisu ya PATH na Chuo kijulikanacho kwa jina la Washington State University's Paul G. Allen School for Global Animal.
"Ziara
hii itadumisha na kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania, “
alisema Mmiliki wa timu hiyo, Joe Roth ambaye pia alisema Kesey na March
watakuwa mabalozi wakubwa wa timu yao katika ziara hiyo.
Alisema
kuwa wajumbe hao pia watatembelea vivutio vya utalii kama Ngorongoro
Crater na jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya Marekani
iliingia katika ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo la
kushughulika na masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.
0 comments:
Post a Comment