SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA
TAARIFA
KWA WANANCHI KUHUSU KUFUNGWA KWA MAUZO YA NYUMBA ZA MAKAZI ZA kIGAMBONI HOUSING
ESTATE ZILIZOKO KIGAMBONI DAR ES SALAAM
Shirika la Nyumba la
Taifa lililizindua mchakato wa mauzo ya nyumba za Makazi za Kigamboni (Kigamboni
Housing Estate) tarehe 20 Desemba 2012, ili kuwapatia Watanzania walioko ndani
na nje ya nchi kupata muda wa kujiandaa kwa ajili ya tarehe rasmi iliyoandaliwa
kwa ajili ya kuanza kupokea rasmi pesa.
Fursa hiyo ililenga kuwapa nafasi pia
watu walioko nje ya nchi, waliosafiri kipindi cha sikukuu na vile vile
ilizingatia maoni ya wateja wetu ambao wamekuwa wakipendekeza kupata taarifa ya
kuanza mauzo kuanzia wiki moja na zaidi ili waweze kijipanga.
Kuanzia tarehe 2
Januari 2013, maombi yalianza kupokelewa na mwitikio umekuwa mkubwa sana. Tumepokea
maombi zaidi ya asilimia 120 ya idadi ya nyumba 182 zinazouzwa. Tunawapongeza
sana wananchi kwa kuitikia wito wa kununua nyumba za makazi za Kigamboni
Housing Estate.
Kama utaratibu wa mauzo unavyotaka, tukishapokea
maombi zaidi ya asilimia 120 lazima tutangaze kufungwa kwa mauzo ya nyumba
husika. Mnamo tarehe 3 Januari 2013 tulifunga rasmi mauzo ya nyumba hizo baada
ya kufikia lengo hilo kwa mradi huu wa Kigamboni kwa sasa.
Tunapenda kusisitiza kuwa
tumefunga zoezi la kupokea pesa kutoka kwa wanunuzi wa nyumba za mradi huu wa
Kigamboni. Hata hivyo, kumalizika kwa mauzo ya nyumba hizi za Kigamboni, ni mwanzo
wa kuanza mauzo ya nyumba za miradi mingine mingi ya nyumba za gharama nafuu
ambayo zinazondelea kujengwa na Shirika hapa Dar Es Salaam na maeneo mengine nchini.
Miradi mingine ya nyumba za gharama
nafuu inayotekelezwa kwa sasa sambamba
na mradi huu wa Kigamboni ni pamoja na Mwongozo Housing Estates (Dar Es Salaam)
na miradi mingine inayoendelea katika Mikoa 14 nchini.
Mikoa na Wilaya zenye
miradi ya nyumba za gharama nafuu kwa sasa ni pamoja na Mvomero (Morogoro), Kongwa
(Dodoma), Ilembo (Katavi), Geita, Mkinga (Tanga), Babati (Manyara), Monduli na
Longido (Arusha), Mkuzo (Songea) na Unyankumi (Singida).
Hivyo, tunawashauri wananchi
waendelee kujiandaa zaidi kwa kuweka akiba ya fedha na vile vile kuendelea kufanya
mawasiliano na benki ambazo zinaushirikiano na Shirika la Nyumba la Taifa ili
waweze kufanyiwa tathmini ya mikopo yao ya nyumba, ili mara tu taarifa za mauzo
ya nyumba katika Miradi zitakapotoka waweze kununua nyumba hizo. Benki ambazo
tunashirikiana nazo ni pamoja na Commercial Bank of Africa (CBA), NBC, NMB, AZANIA
BANK, BANK OF AFRICA(BOA) na Banc ABC. Benki zingine ni EXIM BANK, KCB na Stanbic
Bank.
Tunawashukuru sana
wateja wetu kwa kutuunga mkono ili kulijenga Taifa letu..
Pamoja Tunaweza
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na
Huduma kwa Jamii.
Shirika la Nyumba la Taifa.
0 comments:
Post a Comment