Nafasi Ya Matangazo

January 04, 2013

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku Nchini (Tanzania Tobacco Control Forum), Lutgard Kagaruki akizindua filamu ya The sixth commandment jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita. Katikati mwenye nguo nyeupe ni Mkurugenzi wa wa Simbeye Film Company na baadhi ya wasanii walioshiriki kucheza filamu hiyo. 
*****
Jina: The sixth commandment au Amri ya sita
Muongozaji: Finnigan wa Simbeye
Urefu: Part I na II jumla masaa 3

Maelezo: Filamu ya The sixth commandment au Amri ya sita inamhusisha msichana mdogo, Catherine Sinda anayecheza kama Maua, binti wa kiongozi wa kanisa ya Yahweh (Mungu) Aliye Juu, Bishop Msemakweli Mkali.

Bishop Mkali nafasi inayochezwa na Finnigan wa Simbeye, mwandishi wa biashara wa gazeti la Daily News, ni kiongozi madhubuti ambaye anaiongoza familia yake kwa umakini mkubwa kama familia ya mfano kufuata matakwa ya Mungu kama ilivyo kwenye maandiko matakatifu ndani ya Biblia.

Maua ambaye ni mwimbaji katika kwaya ya vijana katika kanisa linaloongozwa na baba yake, anapata virusi vya Ukimwi kwa bahati mbaya wakati akimuhudumia rafiki yake, Mrs Poa ambaye ni mke wa Mchungaji Babalao Poa msaidizi wa Bishop Mkali kanisani.

Mrs Poa aliumia wakati akitoka dukani kununua vinywaji kwaajili ya ugeni wa wanakwaya wenzake na Maua waliokuja nyumbani kumuona Pastor Poa ambaye ni mlezi wa kwaya ya vijana ya kanisa la Yahweh.

Akijaribu kumhudumia Mrs Poa, Maua anajisahau kwamba naye ana kidonda kibichi alichoumia siku chache tu wakati akikata viungo, na kwahiyo kuruhusu damu ya rafiki yake igusane na yake.

Kwa Bishop Mkali kila aliyeathirika na Ukimwi ni mzinzi ambaye adhabu yake stahiki ni kifo na kwahiyo Maua anastahiri adhabu hiyo kwa kukiuka mafundisho ya Biblia na familia yake. Maua anashindwa kuhimili manyanyaso ya baba yake huyo na kuamua kujiua kwa kumeza vidonge.
Posted by MROKI On Friday, January 04, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo