Mahakama ya Wilaya Kongwa Jana ilimuhukumu Bw. Jumanne Hassan Miaka
(22) mkazi wa kijiji cha Liganga, Kata ya Chitego tarafa ya Nzoisa wilayani
humo kutumikia kifungo cha miaka (30 ) jela na kuchapwa viboko (12) baada ya
kumtia hatiani kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa darasa la tano.
Mwandesha mashtaka, Mkaguzi Wa Polisi Maulid Manu aliiambia Mahakama hiyo kuwa Bw.
Jumanne Hassan alimbaka binti mwenye umri wa miaka (12) ambaye jina lake
limehifadhiwa na ni mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Liganga
iliyopo wilayani kongwa.
Mwendesha mashtaka huyo wa Polisi, aliieleza mahakama kwamba Bw.
Jumanne Hassan alitenda kosa hilo kwa kumvizia binti huyo aliyekuwa anatoka
kununua mahitaji ya dukani alipokuwa ametumwa kisha kumkamata mkono na kumvutia
katika chumba cha rafiki yake kilichokuwa jirani na eneo hilo kisha kumbaka na
kumtishia kwamba akipiga kelele atamuua.
Alieleza hayo mbele ya mbele ya hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Kongwa
Bw. Godfrey Pius, aidha alisema tukio hilo lilitokea Novemba moja, mwaka jana
(2011) majira ya sa mbili na nusu usiku katika eneo la kijiji cha Liganga, Kata
ya Chitego na Tarafa ya Nzoisa Wilayani Kongwa.
0 comments:
Post a Comment