Nafasi Ya Matangazo

December 17, 2012

 
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Azania wakiwa katika mchezo wa mpira wa miguu wakati wa siku yao ya Michezo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa bahari katika Hoteli ya Jangwani Sea Breeze iliyopo jijini Dar es Salaam
*****
BENKI ya Azania ya Tanzania imesema kuwa michezo ni muhimili unaosaidia kuimarisha afya, kuleta umoja na kukuza utendaji kazi wa watu katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya kibenki. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Bw. Charles Singili, wakati wa hafla ya wafanyakazi wa benki hiyo ya mwaka 2012 iliyowakutanisha wafanyakazi wa makao makuu na matawi yake yote yaliyopo Dar es salaam. 

Wafanyakazi hao walishiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa wavu, kuogelea pamoja na kucheza muziki, tukio lililofanyika mwishoni mwa wiki katika ufukwe wa bahari katika hoteli ya Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam. “Hili ni tukio muhimu sana kwetu kama Benki ya Azania kwa kuwa tunahitaji wafanyakazi wetu kuwa katika afya nzuri kimwili na kiakili na tunatambua kuwa kupitia michezo tutaendelea kuwa na wafanyakazi wenye afya nzuri na wataweza kuongeza juhudi katika utendaji kazi wao na kuleta umoja ndani yetu. 

 “Matukio kama haya yanayokutanisha wafanyakazi wetu, yanatusaidia katika kufahamiana vizuri, kubadilishana mawazo na kutafakari kwa umoja wetu nini tufanye zaidi katika kuhudumia wateja na kukuza huduma zetu na kuleta tija zaidi katika sekta ya kibenki,” alisema Bw. Singili. 

Alisema kuwa baada ya kufanyakazi mwaka mzima wakiwa wanahudumia wateja wao na kuwasaidia kufikia malengo yao kwa kuwapatia huduma za kifedha na za kibenki, benki hiyo iliona ni vyema kupata japo siku moja ya kushiriki katika michezo na wakati huo huo kuweza kutafakari kwa pamoja ni jinsi gani benki itaongeza tija katika kuwahudumia wateja pamoja na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi kwa ujumla. 

“Benki ya Azania haishiriki katika michezo tu lakini pia inasaidia makundi mbalimbali ya kijamii katika mahitaji ya kiafya, kielimu na kutoa misaada kwa mayatima na makundi mbalimbali ya wasiojiweza. Tunatoa michango yetu tukitambua umuhimu wa makundi haya katika kusaidia kujenga Taifa letu,” mkurugenzi huyo alisema. Bw. Singili aliongeza kuwa benki hiyo hutoa misaada hiyo ikiwa ni kama jukumu la benki katika kuirudishia jamii sehemu ya mapato yake wakati benki inatengeneza faida.
Posted by MROKI On Monday, December 17, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo