Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya ya
Afrika Mashariki wakikata utepe kwa pamoja kuzindua rasmi wa Barabara
ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa
upande wa Tanzania.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo
na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan
(kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini
Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012.Rais Kikwete yupo nchini Kenya
kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya
Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya
miundombinu.Wengine Pichani ni Rais wa Kenya,Mh. Mwai Kibaki (katikati)
na Rais wa Burundi,Mh. Nkurunzinzah.
Wakati wa Wimbo wa Taifa.
Baadhi ya
mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za
uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu
wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la nchini Kenya wakiwa kwenye Sherehe hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wenzie wa nchi wanachama za Jumuiya
ya Afrika Mashariki wakipata maelezo ya Barabara hiyo itakavyokuwa
kutoka kwa Injinia.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika uzinduzi rasmi wa Barabara ya
Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande
wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment