NA
Andrew Chale
MWANDISHI
wa Habari wa kituo cha SIBUKA, aliekuwa akitangaza na kuandaa vpindi mbalimbali
kikiwmo cha Pepeta frika, Lulu Oscar (pichani)amefariki dunia leo nyumbani kwao
Mbezi Kwa Yusufu.
Akizungumz na Tanzania Daima, mdogo wa marehemu, Ritha Oscar alisema kuwa Lulu alipatwa na mauti hayo majira ya usiku ambapo alizidiwa ghafla kufuatia kulalamikia kifua kumbana.
“Awali alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Masister ya Luguluni kule Mbezi, zaidi ya mara tatu, jana aliruhusiw kurudi nyumbani lakini baada ya kuendelea vizuri lakini jioni usuku alilalamikia kifua kikimbana tulimuangaikia mpaka hatua ya mwisho lakini ikashindikana na alipoteza maisha” alisema Ritha kwa masikitiko makubwa.
Ritha alisema kuondoka kwa Lulu kwenye familia yao ni pigo kubwa kwani alikuwa bado ni mdogo na alikuwa msaada mkubwa kwa ndugu na jamaa.
Aidha, alisema kuwa, kikao cha muda cha ndugu kilichokaa wameafikiana kuzikwa siku ya Alhamisi katika Makaburio ya Kinondoni. “Mpaka sasa taarifa za familia, ni kuwa mazishi yatakuwa siku ya Alhamisi pale mkaburi ya Kinondoni na msafara utaanzia nyumbani Mbezi kwa Yusufu na kuelekea Makaburini” alisema Ritha.
Marehemu alikuwa mwajiliwa wa televisheni ya SIBUKA (TV SIBUKA) akiwa kama mtangazaji na mwandaaji wa vipindi ambapo pia alikuwa akiandaa na kutangaza kipindi cha Pepeta Afrika, kilichojizola umaarufu mkubwa mpaka anakufa kwake.
Katika historia yake, Lulu alihitimu elimu yake ya msingi alihitimu mwaka 1996 katika shule ya Upanga na kwa elimu ya uandishi wa habari alisomea chuo cha Royal College of Tanzania na baadae mwaka 2003, aliweza kuhitimu kozi zake hiyo ya juu katiika Taasisi ya uandishi wa habari na mawasiliano Institute of journalisim and mass communication.
Marehemu alikuwa hajaolewa wala hajaacha mtoto.
0 comments:
Post a Comment