Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa.
Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu (Bara)
Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) |
Nape Nnauye, abakia katika Nafasi yake ya Katibu wa Itikadi na Uenezi.
Dr. Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha.
Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni.
LICHA ya aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM, Abraham Kinana, kusesema hatogombea tena nafasi za
vikao vya juu vya CCM kwa kuwa muda wa 25
wa kukitumikia chama hicho kama kiongozi unatosha lakini Kinana ameteuliwa kuwa
Katibu Mkuu wa Chama hicho kushika nafasi ya Wilson Mkama.
Taarifa kutoka
ndani ya CCM zinasema Abraham Kinana ndiye Katibu Mkuu huku nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara ikichukuliwa
na Mwigulu Mchemba, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Katibu wa Uenezi na Itikafi anaendelea Nape Nnauye, Katibu
wa Uchumi na Fedha amerejeshwa Zakhia Hamdan Meghji, Katibu wa Organizesheni ya Mohamed Seif
Khatib na Katibu wa Mahusiano na Mambo ya Nje ni Dk. Asha Rose Migiro.
Jana jioni
wajumbe wa mkutano Mkuu wa nane wa CCM uliomalizaka mjini Dodoma walimrejesha
madarakani Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete kwa kura 2395 sawa na
asilimia 99.92 kati ya kura 2397 zilizopigwa.
Aidha wajumbe
hao wapatao 2397 waliopiga kura waliwachagua Philip Mangula kuwa Makamu
Mwenyekiti Tanzania bara na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.
Baadhi ya wadau
na wanachama wa chama cha Mapinduzi wanapasha kuwa Kinana utakisaidia sana
chama akiwa Katibu Mkuu wa CCM na chama kitakuwa katika mstari mzuri.
Pia wamesema
kuwa kwake Katibu Mkuu kutamfanya kuyatekeleza na kusimamaia vyema mapendekezo
yote aliyokuwa akiyatoa jana kabla ya kufungwa kwa Mkutano huo mkuu.
0 comments:
Post a Comment