Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2012

Wachezaji wa Kilimanjaro Stars wakitoka Uwanjani baada ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Makerere Kampasi ya Biashara nchini Uganda jana. Kilimanjaro Stars, ipo nchini Uganda kushiriki michano ya mwaka huu ya Tusker Challenge Cup.
Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars, Edward Christopher akikokota mpira wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Makerere Kampasi ya Biashara nchini Uganda jana kwa kujianda na mchezo wa michuoano ya Tusker Cecafa Challenge . Stars inadhaminiwa na Bia yaKilimanjaro Premium Lager
********
Na Mwandishi wetu, Kampala
Kocha wa Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Kim Poulsen amesema ana imani na timu yake itakayotupa karata ya kwanza leo (Jumapili) dhidi ya Sudan katika mashindano ya Tusker CECAFA Challenge 2012.

Alisema suala la wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kutofika mpaka sasa halimtatizi kwa kuwa ameiandaa timu vizuri na atawatumia wachezaji waliopo.

“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaweza wasicheze katika mechi ya kesho kwa sababu hawajafika lakini mimi nikiwa kocha nimejiandaa vizuri na nina imani na wachezaji waliopo,” alisema.

“Nina imani TFF wanafuatilia suala hili na wachezaji hawa watajiunga na wenzao hivi karibuni lakini hii haituzuii kufanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri,” alisema.

Kuhusu wachezaji kama Aggrey Morris, Mohamed Nassoro na Mwadini Ali kutoka Zanzibar kujiunga na wenzao kuichezea Zanzibar Heroes, Poulsen alisema pengo lao halitampa tatizo kwa kuwa ni hangamoto.

“Timu hii ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa sasa ina wachezaji wengi chipukizi kwa hivyo huu ndio muda wa kuwapima vizuri kwani kwani haya ni mashindano makubwa,” alisema.

Alisema wachezaji wote wana hali nzuri na wana ari ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Sudan ambazi zimo katika Kundi B pamoja na Burundi na Somalia ambazo zitacheza leo pia.

Timu za kundi A zilitarajiwa kucheza jana ambazo ni Kenya dhidi ya Uganda na Ethiopia dhidi ya Sudan Kusini. Kundi C inajumuisha Zanzibar na Eritrea na Rwanda dhidi ya Malawi.
Posted by MROKI On Sunday, November 25, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo