Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2012

Mwenyekiti wa Msikiti wa Jamaat Shia Ithna Asheri Bw. Azim Dewji akifafanua kwa waandishi wa habari amesema katika kuadhimisha siku hii Waislam wa dhehebu la Shia watafanya matembezi kutoka makaburi ya Shia Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia Ithna Asheri na wakati wa matembezi hayo ndani yake kutakuwa kunafanyika kumbukumbu kwa njia ya kuimba nyimbo za maombolezo tukikumbuka shujaa wetu namna alivyouwawa na vile vile sisi kujipa uhai kiroho katika kuonyesha namna kiongozi anaweza kujitolea kwa watu wake na kwamba ni funzo kwa kila mwanadamu ajitolee kwa ajili ya wenzake.
Imamu wa Msikiti wa Imam Ali wa Magomeni Mapipa Msabaha Shaaban Ali Mapinga akizungumza na waandishi wa habari amesema siku hii ni siku ya kukumbuka na kuadhimisha miaka 1473 ambapo katika nchi ya Iraq kwenye mji wa Karbala aliuwawa mjukuu wa Mtume Mohammed (S.A.W) aliyekuwa akijulikana kwa jina la Imam Hussein Bin Ali Bin Abutwalib.

Amesema katika nyakati hizo alitokea mtawala dhalim aliyekuwa akitetea dhulma na kukiuka haki za binadamu kitendo ambacho mjukuu wa Mtume Imam Hussein hakukubaliana nacho na kuunda jeshi lake dogo kutetea haki na kupinga Batili.

Kwakuwa Imam Hussein alikuwa na dhamana ya kutetea haki alikataa kuwa chini ya mtawala huo ndipo alipotumiwa jeshi la watu kama 30,000 naye akiwa na jeshi la watu 72 walipambana katika mji huo na mjukuu wa Mtume aliuwawa kifo cha kikatili cha kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
Kwa Upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema siku hii ni muhimu sana kwa Waislam kote duniani kwa sababu tunamkumbuka Imam Hussein ambaye kifo chake kilikuwa ni kifo cha kinyama, kifo cha wapenda dhulma katika uso wa ardhi.

Amesema kifo cha Imam Hussein kinamgusa kila Muislam kwa sababu ilikuwa ni siku ambayo haki ilizimwa na dhuluma, maadui wa haki walijaribu kuitaka batil isimame , kwa hiyo siku ya leo ni sku ya kutetea haki na uadilifu.

Aidha Sheikh Salum amesema kwa Waislam wote Tanzania na hata wasio Waislam wanatakiwa wajifunze kutoka kwa Imam Hussein kwamba yeye alikuwa ni mtetezi wa haki, alikuwa anatetea Uadilifu kwa hiyo tujifunze kwamba kutetea haki na kutetea uadilifu ndio jambo linalotakiwa katika maisha ya leo, kutetea wanyonge, kupiga vita Dhuluma na ukandamizaji wa namna yoyote ile ndio lililokuwa jambo alilolipenda Imam Hussein.
Waumini hao wakiwa wamejipanga tayari kuanza maadamano kutoka makaburi ya Kisutu hadi katika msikiti mkuu wa Shia.
Pichani juu na chini msafara wa waumini wa Shia umeanza.
       
Hisia na Majonzi vilionekana.
 
Ni jambo jema watoto kujua dini mapema, kama inavyoonekana pichani mtoto akiwa ameambatana na mzazi wake katika maandamano ya siku ya Ashura.
Bango lenye Ujumbe maalum wa siku ya Ashura.
 
Posted by MROKI On Sunday, November 25, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo