Mama wa
Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia Kampuni yake ya Fabak
Fashions wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale litakalofanyika
Novemba 23, 2012 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Onyesho
hili kubwa ambalo limekuwa likifanya vizuri kwa takribani miaka minne
sasa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania hasa katika
nchi ya Marekani, litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka sehemu
mbali mbali ambao nao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.
Watu
Maarufu hapa nchini watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha Mavazi ya
Khanga za Kale kutoka kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ambapo
fedha itakayopatikana kutokana na onyesho hilo imepangwa kupelekwa
kwenye Kituo cha Kulea watu walioathirika na Madawa ya Kulevwa kilichopo
Kikale Wilayani Rufiji, Mkoani Pwani.
0 comments:
Post a Comment