Nafasi Ya Matangazo

November 12, 2012

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe, wakati alipowasili katika hafla ya chakula cha jioni katika yake, Balozi na maaofisa wa Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ili kuagana na kutathimini mapungufu na mafanikio ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya dunia ya utalii World Treavel Market (WTM) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Uingereza, ambapo zaidi ya makampuni 55 yanayouza na kutangaza utalii wa Tanzania yalishiriki katika maonyesho hayo, maonyesho hayo hufanyika kila mwaka eneo la Excel jijini London.

Balozi Khamis Kagasheki aliitaka Bodi ya Utalii Tanzania kuongeza juhudi zaidi ili kuleta mafanikio zaidi katika maonyesho hayo na menine na kuongeza idadi ya watalii kufiki milioni moja kwa mwaka, Tanzania ikijipanga vizuri na kutangza vivutio vyake zaidi duniani inaweza kupata mafanikio zaidi katika utalii na kuongeza zaidimapato yake ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii. PICHA NA WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliwashukuru maofisa kutoka Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo kwa maandalizi mazuri katika ushiriki huo, lakini pia akaagiza kuangalia changamoto na kuzifanyia kazi ili kuboresha zaidi ushiriki wa Tanzania katika maonyesho yajayo na mengine yanayoweza kufanyika katika nchi zingine, kulia katika picha ni Balozi Peter Kallaghe na kulia ni Mama Balozi
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe akizungumza katika hafla hiyo kulia ni Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili na Utalii.
Baadhi ya maofisa waliohudhuria katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Dkt. Wegoro kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha , Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Balozi mdogo wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Kilumanga na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania ubalozini Bw. Kashangwa.
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Meena wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na maofisa kutoka TANAPA, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza katika hafla hiyo.
Maofisa mbalimbali wakiingia katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.
Maofisa kutoka TANAPA na Ngorongoro wakiwa katika hafla hiyo.
Ofisa Habari wa TANAPA Bw. Shelutete kulia akiwa na Maofisa wa Kituo cha biashari cha Tanzania nchini Uingereza katikati ni Dilunga na kushoto ni Mohamed
Maofisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakiwa katika hafla hiyo.
Wadau wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya kufungwa rasmi kwa maonyesho hayo kutoka kulia ni Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw, Geofrey Meena, Mdau Angela Msangi kutoka Shirika la Utangazaji TBC, Juma Mabakila kutoka Jambo Concerpt na Mama Juma Pinto
Mdau Hafsa Omary kulia akiwa na wadau wengine watanzania wanaoishi nchini Uingereza ambao walihudumu katika banda la Tanzania wakati wote wa maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza mara baada ya kufungwa kwa maonyesho hayo yaliomaliziki mwishoni mwa wiki, aliyeshika kinasa sauti ni Hafsa Omary aliyewahi kufanya mazoezi ya mafunzo ya uadhishi wa habari TBC hapa akikumbushia enzi zake.
Mh. James Lembeli Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Maliasili, Utalii na Ardhi akitoa machache mara baada ya kumalizika kwa maonyesho hayo wakati akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa TBC nchini Uingereza, ambapo aliiomba bodi ya utalii kufanya jitihada za maksudi kuwahamasisha na kuongeza idadi ya washiriki wazawa wa Tanzania katika maonyesho hayo
Nami nikapata japo picha moja na mdau Hafsa Omary mara baada ya kukamizika kwa kazi nzima ya kuripoti matukio ya maonyesho hayo yaliyomaliziki mwishoni mwa wiki iliyopita jijini London nchini Uingereza.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kulia akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maliasili, Utalii na Ardhi wakati alipokuwa kichangia mazungumzo katika hafla ya chakula cha jioni baada ya kumalizika kwa maonyesho ya WTM nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita, katikati ni Balozi wa Tanzania nchini humo Balozi Peter Kallaghe.
Posted by MROKI On Monday, November 12, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo